Panya Road ni zao la mfumo mbovu wa elimu, na Watawala kutokujali

Panya Road ni zao la mfumo mbovu wa elimu, na Watawala kutokujali

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2022
Posts
389
Reaction score
757
South Africa ina moja ya Jeshi la Polisi lenye vitendea kazi bora kabisa kwa Bara la Afrika lakini angalia uhalifu.

Hawa Panya Road tunajidanganya wataisha kwa kuongeza nguvu na kumwaga polisi wa kutosha mitaani, hii ni zima moto tu, je chanzo cha hao panya road ni kipi? Je, watawala wana dili na chanzo?

Hawa panya road ni zao la shule za Kata, vijana wanatoka pale wanarudi mtaani hakuna cha kufanya, Hakuna viwanda vya kutosha kwamba wataenda hata kufanya unskilled job, na haiwezekani wote hao wawe wamachinga.

Hii panya road ni genge na huko mbele yatakuja ibuka magenge mengi sana na hapatakalika, South Africa si ilianza hivi hivi? Ule uhalifu wa South Africa si Polisi wao wana nyenzo? Ila wameshindwa. Hili lipo pia Nairobi Kenya.

Wabunge kule Bungeni badala wajadili mambo magumu kwa ajili ya hii nchi wako bise wanajadili vilimo vya bangi na kuruhusu wafungwa wawe wanapiga miti. Tatizo la elimu duni na pia kukosekana kwa ajira na hizi ajira chache za kujuana ndio zinazaa hawa panya road.

Hao wengi ukifuatilia utashangaa ni Form four leaver sasa watafanya nini? Hawajaweza kuendelea na kidato cha 5 na shuleni hakuna ujuzi wametoka nao kwa hiyo miaka yote ya elimu ya msingi pamoja na secondary.

Hii suala halitamalizwa kwa Polisi kujazwa mitaani.
 
Wabunge kule Bungeni badala wajadili mambo magumu kwa ajili ya hii nchi wako bise wanajadili vilimo vya bangi na kuruhusu wafungwa wawe wanapiga miti. Tatizo la elimu duni na pia kukosekana kwa ajira na hizi ajira chache za kujuana ndio zinazaa hawa panya road.
Ulitaka wajadiliane nini wakati wanajua wapo kule kwa 'ridhaa ya chama chao' na sio 'ridhaa ya wapiga kura'!
 
Na suluhu waliyo nayo ni kujenga uchumi wa tozo, yaani muue sekta binafsi mtegemee maendeleo! kule kwingine wakaua sekta ya usafiri wa anga wakitaka kufufua shirika lao ambalo sasa limekuwa mzigo kwa walipa kodi........mnaishia kukamua watu maskini na middle class hata kile kidogo walicho nacho.​
 
South Africa ina moja ya Jeshi la Polisi lenye vitendea kazi bora kabisa kwa Bara la Afrika lakini angalia uhalifu.

Hawa Panya Road tunajidanganya wataisha kwa kuongeza nguvu na kumwaga polisi wa kutosha mitaani, hii ni zima moto tu, je chanzo cha hao panya road ni kipi? Je, watawala wana dili na chanzo...
nadhani pamoja na kuwa na mifumo mibaya ya elimu na ajira mimi bado ni mwumini wa amani.vitendo vya uvunjifu wa amani havikubaliki hakuna mtu mwenye ithibati ya kuvunja sheria ati kwa sababu hana cha kufanya.

Serikali pia haiwezi kuajiri wahitimu wote wa nchi hii pamoja na mapungufu yaliyopo ndani ya taasisi zetu za serikali.kuna mambo mengi ya kufanya na ukajipatia kipato bila kuvunja sheria.

Kuna biashara ndogo ndoogo ambazo hata mitaji yake si mikubwa sana ambazo zinaweza kuwapatia kipato.kuna shughuri za ufundi unaweza kujiweka kwa mtu na akakupa ujuzi tena kwa gharama nafuu pengine hata bure.si vizuri kuwahasisha vijana waingie kwenye vitendo viovu bali tuwasaidie kuachana na vitendo hivyo.
 
Hawa panya road ni zao la shule za Kata, vijana wanatoka pale wanarudi mtaani hakuna cha kufanya, Hakuna viwanda vya kutosha kwamba wataenda hata kufanya unskilled job, na haiwezekani wote hao wawe wamachinga.
Hawa panya road pia ni zao la watoto wanaozaliwa bila ya uangalizi. Kila siku humu munakuja kujisifu kwenye mitandao munavyotembea na vibinti (tena bila kinga), matokeo watoto wanazaliwa bila uangalizi wa mzazi.

Haraam kumleta mtoto duniani bila ya kumshughulikia.
 
Back
Top Bottom