Panya wamevamia kilimo cha mahindi mwaka huu

Political Engineer2

Senior Member
Joined
Feb 23, 2018
Posts
149
Reaction score
117
Naona kila mwaka na janga lake kwenye kilimo.Mwaka Jana mavuno yalipatikana lakini janga likawa bei kushuka mpaka kufikia gunia kuuzwa 20,000tsh.

Mwaka huu tumeshambuliwa na panya wanakula mbegu ardhini mpaka sasa hatujajua cha kufanya,wengine wanarudishia zaidi ya Mara tatu.

Tatizo kubwa ni kuchelewa kwa mvua ukilinganisha mwaka Jana .

Kyamyorwa ni kilio mwaka huu. Je huko kwenu vipi?

Naomba kuwasilisha.
 
Weka sumu ya panya

Roweka mbegu zako masaa 12 kisha zitoe zifunge kwenye kanga ama tenge ,zitie kwenye ndoo masaa 24 zitakuwa zimeanza kupasuka kaoteshe hakuna panya atakayefukua asilani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…