Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, amefichua siri kuwa Watu walipanga kumuua wakati akiwa safarini nchini Iraq March 2021 lakini mauaji hayo yalizuiwa baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kutoka Nchini Uingereza.
Papa amefichua njama hizo za jaribio la mauaji yake kwenye kitabu cha maisha yake kinachoitwa ‘Hope’ ambacho kinatarajiwa kuchapishwa January 14,2025 ambapo amesema baada ya kutua Baghdad mwezi March 2021, aliambiwa kuhusu tukio hilo ambalo lilipangwa kutekelezwa na Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga ambao wote walikamatwa na kuuawa.
Sehemu ya kilichomo kwenye kitabu chake hicho imechapishwa na gazeti la Italia Corriere della Ser ambapo pamoja na mambo mengine imeeleza kuwa wakati anajiandaa kuifanya ziara yake hiyo ya siku tatu Iraq wakati wa janga la corona, kila Mtu alimshauri asiifanye lakini aliona ni bora aifanye na kusema sababu ya kuambiwa asiende Iraq ni kufuatia Nchi hiyo kukumbwa na ongezeko la ghasia za kimadhehebu na mapigano kati ya Waislamu wa Shia na Sunni pamoja na mateso ya dini ndogo na kupelekea Jumuiya ya Wakristo Nchini humo kupungua kwa kiasi kikubwa wakati huo baada ya kulengwa hasa na kundi la Islamic State na Wafuasi wengine wa itikadi kali za Kisunni.
Amesema njama hiyo ya kutaka kuuawa ilifichuliwa na Majasusi wa Uingereza, ambao walionya Polisi wa Iraq na wao kwa upande wao walimweleza maelezo yake ya usalama mara tu alipowasili “Mwanamke aliyejaa vilipuzi, kijana mlipuaji wa kujitoa mhanga, alikuwa akielekea Mosul kujilipua wakati wa ziara yangu na gari pia lilikuwa limeondoka kwa kasi kubwa kwa nia hiyohiyo.”
Papa amesema alimuuliza Afisa wa Usalama siku iliyofuata nini kimewapata Washambuliaji hao na alijibu kwa unyonge “Hawapo tena, Polisi wa Iraq walikuwa wamewakamata na kuwalipua”