Papaa Musofe mbaroni kwa mauaji!

kwa uarifu wa aina yoyote Bongo-Papaa Msofe,Alex Massawe na Said Saad (mmiliki wa Home Shopping Center),nani ni the DON? kwa maana ya nani zaidi?
 


Pia maeneo ya Sinza kuna watu walilizwa sana kwa mtindo huu lakini sina uhakika kama ni huyu jamaa. Analipwa jioniii usiku wanakuja watu wanamweleza kuwa una kiasi fulani tupe bila kupunguza hata shilingi. NI HATARI!!!!!!!!!!!!.
 
kwa wengi msiojua mambo ya mjini huyu jamaa ni mtu mukubwa kwa kweli pesa iko kwa mali ninazojua mimi hana nyumba kama 50 jamaa kawekeza sana kwenye nyumba upanga nyumba 4 na mbezi 7 bado mikocheni na zote ziko powa mwananyamala na kinonondoni usiseme then ni mafia hatari kwa mnaofikiri anaweza kufungu sahau hii nchi ni hela ndio mpango mzima.
 

Dah...mdau uko makini...ilikuwa wapi hapo?
 

Alilikata mikono nini?

 
Hapana huyu ni Legrande Mupao suvereee mwokonzi Papa musofe mutu ya pakee,mutu ya pesa mingi......Ndama mutoto ya ngombe na musofe ni category hyo hyo ya wapigaji(conmen),matapeli wa mujini!

Lol, jamani I love JF!
 
Dah, unajua ni pigo kubwa sana?

Yaani hapa nawaza nikatafuta hata kazi ya kuuza genge.

Ila janmani, mwanamke midhahabu, na mwanamme midhahabu lol

Kongosho, chonde chonde...mwanamke midhahabu mwanaume dhahabu. Kisa cha kujipamba vile nini?
 
Jamaa siku za karibuni alikuwa serious sana na mazoezi. Labda ilikuwa ndio maandalizi maana huwa wanaambiwa mapema mchezo wote unavyokwenda.
 
Lakini inawezekana mapolisi wamefanya hivyo hili wapate fedha si unajua mpaka leo tar 33 hawajapewa mshaara? Jamaa kwa kukata hela huyu ni nomaaaaa kuna ndugu yake mwanajeshi wa navy(Mfinanga) alishawahi kuua mtu kwa risasi na pia alishawahi kukamatwa kwa ujambazi lakn papa musofe alikata hela na akamtoa sembuse yeye? Jamaa atatoka tu coz kuna askari wapo kwenye payroll yake!
 
huwa sikuaminiga King Kong III ila katika hili, mh... maana issue lenyewe ndio limeishia!

 
Haya magenge ya ki-mafia ya kina papaa msofe na alex masawe kama serikari haina uwezo wa kuyatokomeza kwa nini tusiombe msaada wa kiintelejensia toka CIA, FBI,MOSAD au Scotland Yard kulinusuru taifa na uhalifu wa aina hii.
 
du, naona kama 'anaonewa' vile!
[h=2]'Papaa Msofe' aswekwa mahabusu kwa mauaji[/h]


Na Hellen Mwango



11th August 2012





Mfanyabiashara maarufu Marijani Abdubakari Msofe maarufu kama 'Papaa Msofe' Akiwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana akiandikisha jalada baada ya kufunguliwa mashtaka ya kesi ya mauaji.


Mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Marijani Abubakari ama Papa Msofe (50), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la mauaji.

Papa Msofe Mkazi wa Mikocheni, alisomewa shtaka lake jana mbele ya Hakimu Mkazi Agnes Mchome wa mahakama hiyo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Tumaini Kweka, alidai kuwa Novemba 6, mwaka 2011, eneo Magomeni Mapipa, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, mshtakiwa anadaiwa kumuua Onesphoty Kitoli.

Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji hadi upelelezi utakapokamilika, kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania.

Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutaja.

Hakimu Mchome alisema kesi hiyo itatajwa Agosti 23, mwaka huu na mshtakiwa apelekwe mahabusu.






CHANZO: NIPASHE
 
Hata kama atatoka kwa pesa, lakini muda atakaokaa huko utamfanya kutafakari kuwa kumbe wakati mwingine pesa sio kila kitu vinginevyo angenunua mtu wa kukaa lumande kwa niaba yake wakati kesi inangojea kupelekwa mahakama kuu!
 
Hizi thread nyingine ni za watoto wa mjini, wewe kama unaishi Mpitimbi hapa huwezi kuelewa kitu. kwanza hujawahi hata kuingia kwenye show ya Ngwasuma unategemea Msofe utamjulia wapi? hawa watu hawatembei mitaani kwenye juwa kali.
Sikujua mkuu Matola
lakini ni nani huyo Msofe?
 
Last edited by a moderator:
Haya magenge ya ki-mafia ya kina papaa msofe na alex masawe kama serikari haina uwezo wa kuyatokomeza kwa nini tusiombe msaada wa kiintelejensia toka CIA, FBI,MOSAD au Scotland Yard kulinusuru taifa na uhalifu wa aina hii.
Hujui unaloliongea.
 

acha kutetea uonevu.ipo siku yao wataomba ardhi ipasuke kwani imeandikwa kila baya litalipwa kwa baya na kila jema litalipwa kwa jema
 
Hizi thread nyingine ni za watoto wa mjini, wewe kama unaishi Mpitimbi hapa huwezi kuelewa kitu. kwanza hujawahi hata kuingia kwenye show ya Ngwasuma unategemea Msofe utamjulia wapi? hawa watu hawatembei mitaani kwenye juwa kali.
tehetehetehetehe umenichekesha kwelikweli huoni hata jina lenyewe .alishaona wapi nyumba inauzwa mara tatu na umeshalipa deni na mtu anakataaa anaiuza tena kwa tapeli mwenzake ili umalizwe khakhaaaa
 
Hizi thread nyingine ni za watoto wa mjini, wewe kama unaishi Mpitimbi hapa huwezi kuelewa kitu. kwanza hujawahi hata kuingia kwenye show ya Ngwasuma unategemea Msofe utamjulia wapi? hawa watu hawatembei mitaani kwenye juwa kali.

Hivi kumfahamu huyo msoffe ni mojawapo ya sifa za kuwa "mtoto wa mjini (Dsm)?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…