Pape Ousmane Sakho transfer updates

Pape Ousmane Sakho transfer updates

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Wawakilishi wa Mchezaji Pape Ousmane Sakho hawaridhishwi na kukosekana kwa muda wa kucheza kwa Mteja wao ndani ya Simba, wakiamini Msenegal huyo anastahili muda zaidi wa kucheza.

Kutokana na hilo kwa mujibu wa taarifa nilizopata ni kuwa kuna baadhi ya ofa watazifikisha Msimbazi kumhusu Mteja wao ambazo zitakuwa na maslahi kwa Simba kiuchumi ili POS aweze kuondoka kusaka changamoto mpya.

POS alisaini kandarasi ya miaka mitatu na Wekundu wa Msimbazi, akiwa ametumikia miaka miwili huku kipengele cha mkataba kikimtaka alipe mshahara wa miezi mitatu tu ili avunje mkataba wake, tayari ameshaandika barua.

Wanaamini Kijana anastahili muda wa kucheza zaidi, ijapo mpaka sasa bado hakuna ofa mezani kwa Simba huku zikitarajiwa mwishoni mwa msimu.

E74ADDF1-F36C-4C8D-BAC8-325A66198326.jpeg
 
... huku kipengele cha mkataba kikimtaka alipe mshahara wa miezi mitatu tu ili avunje mkataba wake, t
Sawa, ni vyema akaangalia sehemu atakapopata muda mwingi wa kucheza, na maslahi pia. Hivi kumbe kipengele cha kuvunja mkataba kwa kuilipa klabu huwa kipo?
 
Simba walikuwa wanakosea jinsi ya kumtumia. Sakho ni mchezaji ambaye walitakiwa wawe wanampa kama dakika 20 za mwisho, atakupa kitu kizuri karibu kila mechi.

Kama watapanga kumtumia hivyo nisingependa kuona akiondoka ila kama ataondoka, itakuwa vizuri kumuona ligi kubwa duniani maana huko wana watu wenye ujuzi wa kuboresha kipaji chake.
 
Unajua maana ya transfer updates???sasa anaenda wapi??mbona hujaandika??au umekopi kwa wachwambuzi uchwala
 
Simba imejaza watu wengi wanaotaka sifa kupitia mgongo wa timu lakini hawana uwezo wa kuiongoza. Sackho, Phiri, Banda na Okra wote ni wachezaji wa kiwango cha juu lakini wanahangaika na watu ambao umri umeshawatupa mkono kama Saidoo na Boko
 
Back
Top Bottom