Pape Sakho aitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Senegal

Qatif

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2014
Posts
379
Reaction score
860
Nyota wa klabu ya Simba Sports, Pape Ousmane Sakho ameitwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 cha timu ya Taifa ya Senegal chini ya Kocha Mkuu Aliou Cisse kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Mozambique.

Sakho ni mchezaji pekee anayecheza ligi za ndani ya Afrika kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Senegal.
 
Nyota wa klabu ya Simba Pape Ousmane Sakho ameitwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 cha timu ya Taifa ya Senegal chini ya Kocha Mkuu Aliou Cisse kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Mozambique.View attachment 2555206
Kupenya kwenye selection ya timu ya taifa ya Senegal siyo jambo dogo. Ameonekana kwa sababu ya uwepo wake Simba.
 
Mioyo,,,Mioyo inaenda mbio sana Simba taratibu kuna watu wanapresha.

Caf super league Simba wamo.
vikosi bora vya caf Simba wamo.
vikosi vya tuzo za caf Simba wamo.
vikosi vya kombe la Dunia Simba wamo.Faamchezo nini,,,!
kwanini Simba tu kwani hii nchi akuna timu zingine?

sisi Yanga roho zinatuuma ni basi tu,ila Mungu yupo.😅😂
 
Utopolo kwa wivu ni hatari, hapa haitapata muda wanasema hili ndo kombe lao Simba

Kwani nyie si mna wachezaji mpaka wamecheza NewCastle Utd hawaitwi huko kwao?!
Kwani makombe hatuna?.yapo mengi tuu waseme lingine
 

Vikosi vilivyopigwa faini na Fifa afu vikazingua kulipa, Yanga wamo
 
Okra kucheza Wodi kapu iliishiaga wapi guvu moya wenzangu ?
 
Makombe matano hayo aisee mwaka wenu huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…