Pape Sakho aitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Senegal

Sijui ni ushamba au ulimbukeni, ajabu ni ipi mchezaji kuitwa timu ya Taifa?
Ni heshima kwa Simba na Utopolo pia, na inafungua milango kwa vilabu vya Afrika na nje pale wanapopitia majina ya Wachezaji walioitwa, haya huwezi kujua kitu kwasababu haya ni mambo magumu kwako labda uwe Sunday au Kikwete.
 
Sijui ni ushamba au ulimbukeni, ajabu ni ipi mchezaji kuitwa timu ya Taifa?
Pamoja na kutofautiana na wewe mara nyingi humu ndani kutokana na tofauti zetu za kishabiki, huwa nakuchukulia mtu fulani mwenye heshima zake. Kuna vitu sitegemei kusikia kutoka kwako.

Ni wiki hii hii tumekuwa na mijadala ya kuhusu uchaguzi wa wachezaji wa Taifa Stars, sikuona ukihoji hilo. Leo Sakho anaenda kuwa katika kikosi cha timu bora Africa, akicheza pamoja na mmoja wa wachezaji bora duniani, akicheza na kikosi kizima cha wachezaji wanacheza Ulaya, halafu unajaribu kushusha umuhimu wa hilo jambo. Kama siyo wivu ni nini?
 
Sijui ni ushamba au ulimbukeni, ajabu ni ipi mchezaji kuitwa timu ya Taifa?
Kuna tofauti kati ya kuitwa timu ya Taifa na kuitwa timu ya Senegal

Senegal unakutana na wachezaji wakubwa akina Sadio Mane (Bayern Munich), Boulaye Dia (Villareal), Bamba Dieng (Lolient) Dialo (Strasbourg) Koulibaly (Chelsea)
 
Kwahio hii nayo ni habari ya kujadili?
 
Kongole kwake Sakho [emoji122]

But Please Simba msije mkaharibu kiwango Cha huyu dogo (maana sikuizii anapata game time ndogo mno, sub kwa sana).

Msije mkaharibu kipaji chake kama mlivyofanya kwa
Ibrahim Ajib
Kibu D
Gadiel Michael

Na awa ambao hawapati nafasi now, (maana nyinyi kila mashindano wachezaji ni walewale)
Kyombo
Kapama
Ramadhani Mussa
[emoji116]Ongezeeni

NB: Maana nyinyi kila mashindano, kila mechi wachezaji ni walewale

Sent from my Infinix X689C using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…