πππ Ila wanigeria bana kwa sifa mbaya waliojiletea wao wenyewe kwa kupenda, usijepata huyo mwamba ni wale Yahoo Yahoo au G Boys. Wale vijana wa kuwalaghai watu hela na mali zao kupitia email, sanasana Yahoo Mail na G Mail. Kuna video niliitizamaa, mzungu alikuwa anatiririkwa na machozi kwenye video call na vijana wa Yahoo Yahoo. Akiwasihi wamrejeshee hela zake eti na alikuwa ameuza hadi nyumba yake na familia yake ndio awekeze kwenye mradi hewa, baada ya wao kumhadaa na kumuingiza box. Alafu jamaa walikuwa wanacheka tu na kumbeza. Eti 'nawaoo you go cry die'. Huwa wanawaita victims wao 'maga' au 'clients'. I go cash out big money o, my maga done pay oo! Mungu awasamehe, umasikini umefanya vijana wawe wahuni.