Parakachoto / Maparakachoto - neno lililobuniwa na Mwanangu Rejoice kutaja Yale yanayoleta kinyaa!

Parakachoto / Maparakachoto - neno lililobuniwa na Mwanangu Rejoice kutaja Yale yanayoleta kinyaa!

Kirchhoff

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,735
Reaction score
8,541
Siku moja kijana wangu wa kwanza mwenye Umri wa miaka minne (Rejoice I. J M) akiwa anaenda shule alikuta ma Pampers yaliyooza barabarani. Aliporudi nyumbani alilalamika kuwa dada yake (housegirl) alimpitisha kwenye Maparakachoto.

Nilipomuuliza dada yake Maparakachoto ni Nini akasema hajui. Kesho yake nikampeleka Mimi. Tukafika mahali akanionyesha maparakachoto. Nikaona ni matakataka yaliyochanganyika na Pampers zilizooza na yanatia kinyaa kweli kweli.

Basi kwa kuwa Mimi na familia yangu tunatumia neno Hilo, nimeona ni vyema na ninyi mlitumie pamoja na familia yangu ili tukuze neno Hilo.
 
Back
Top Bottom