Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUMBUKUMBU KIFO CHA MANGI MKUU THOMAS MAREALLE 14 FEBRUARY 2007: PARAMOUNT CHIEF THOMAS MAREALLE KATIKA NYARAKA ZA RAJABU IBRAHIM KIRAMA WA MACHAME NKUU
Mara yangu ya kwanza kusoma historia ya Mangi Mkuu Thomas Marealle ilikuwa ndani ya Nyaraka za Sykes wakati natafiti kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.
Kwa bahati mbaya sikuweza kutumia yale niliyosoma katika kitabu nilichokuja kuandika kwa kuwa mengi katika yale niliyosoma yaikuwa mambo binafsi zaidi kuliko historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ingawa jina la Nyerere lilikuwa likijitokeza.
Nimekuja kukutana tena na Mangi Mkuu Thomas Marealle baada ya kiasi cha miaka 30 kupita katika Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama wakati natafiti maisha ya Mzee Rajabu wa Machame Nkuu.
Napenda kama kumbukumbu ya kifo cha Mangi Mkuu nieleze machache katika yale ambayo nimejifunza katika kusoma barua walizokuwa wakiandikiana watu hawa wawili kutoka Kilimanjaro kila mmoja akiwa na nafasi muhimu katika jamii ya kabila la Wachagga.
Thomas Marealle akiwa kwanza Mangi wa Marangu kisha Mangi Mkuu wa Wachagga, Rajabu Kirama yeye akiwa kiongozi wa Waislam na mtu aliyeueneza Uislam Uchaggani akianzia harakati zake kijijini kwake Machame Nkuu katika miaka ya 1930.
Harakati hizi zilileta uadui mkubwa kati yake na Chief Shangali.
Mwishoni wa miaka ya 1800 Wajerumani baada ya kuchoshwa na vita visivyokwisha baina ya Wachagga wenyewe kwa wenyewe waliamua kuwakamata takriban mangi wote isipokuwa Shangali na Marealle.
Jumla ya mangi 19 walinyongwa hadharani isipokuwa Chief Marealle na Chief Shangali.
Haya ndiyo madhila yaliyowakumba Wachagga chini ya utawala wa Wajerumani.
Watoto wa machifu hawa wawili hata hivyo walikuja kupata nguvu kubwa sana katika utawala wa Waingereza.
Katika utawala wa Waingereza na katika hali ya amani na utawala Wachagga waliunda chama - Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU) (Umoja wa Raia wa Kilimanjaro).
Petro Njau akiwa kiongozi wa chama hiki alipewa jukumu la kusimamia maslahi ya Wachagga kama taifa.
Katika kanuni za KCCU kanuni hizi zinawataja Wachagga kama watu waliozaliwa huru na wenye haki ya kulinda uhuru wao.
Petro Njau alikinadi chama hiki kuwa ni ‘’chama cha siasa cha kikabila.’’
Nilipokuwa nasoma Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama nilishangaa sana kusoma kuwa Wachagga kwa asili waliichukulia Kilimanjaro yote kuwa ni nchi.
Nyaraka za KCCU zimejaa maneno ya itikadi ya: ‘’nchi,’’ ‘’taifa,’’ ‘’raia,’’ ‘’uchaguzi,’’ ‘’kura,’’ na ‘’utawala.’’
Petro Njau Rajabu na Ibrahim Kirama walikuwa wanaunganishwa na kukubaliana katika jambo moja kubwa na muhimu sana katika utawala wa Wachagga nalo ni kuwa Mangi walikuwa na nguvu zilizopea wakati raia wao hawakuwa na sauti yoyote.
Kwa ajili hii basi wanastahili kuondolewa wote na awekwe kiongozi mmoja tu atakaetawala Kilimanjaro yote na Wachagga wote.
Petro Njau alikuwa mwandishi wa Mzee Rajabu na pia mwandishi wa Chief Thomas Marealle pale Kilimanjaro ilipokuwa katika siasa za uchaguzi kutafuta Mangi Mkuu atakaekuwa juu ya Mangi wote, yaani Paramount Chief.
Rajabu Kirama alisimama bega kwa bega na Petro Njau katika fikra hii.
Thomas Marealle na Abdiel Shangali ndiyo walikuwa wanagombea nafasi ya Mangi Mkuu na bahati mbaya sana kwa Abdiel Shangali ni kuwa alikuwa na uadui mkubwa na Rajabu Ibrahim Kirama.
Rajabu Kirama akasimama kumsaidia Chief Marealle awe kiongozi wa Wachagga wote.
Hivi ndivyo Thomas Marealle alivyokuja kuchaguliwa kuwa Paramount Chief, yaani Mangi Mkuu.
Picha: Mzee Rajabu Ibrahim Kirama, Mangi Mkuu Thomas Marealle wa Marangu na Chief Abdiel Shangali wa Machame.