Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #21
Schmidt,Home-cooked garbage.
Schmidt,Quit the BS, Mzee MS. Only fools would believe any of your tales , spins and half-truths.
Let’s agree on one simple thing: You’re a fake historian, Mzee MS. You can never be taken seriously in anything you write. You’re a fraudster. A pretender.Schmidt,
Hapana huu uwanja uko huru kwa yeyote kuchangia fikra zake.
Sasa wewe kunifukuza kuwa nisiwepo hapa barzani si haki.
Anaetakiwa kujiondoa hapa ni wewe si mie.
Wewe ndiyo hupendezewi na kalamu yangu.
Huna haja ya kujiumiza bure na ukawa unatukana.
Uachotakiwa kufanya ni kuacha kunisoma.
Ikiwa wewe huamini haya niandikayo hapana ugomvi wako wanaoelemika na kalamu yangu.
Schmidt,Let’s agree on one simple thing: You’re a fake historian, Mzee MS. You can never be taken seriously in anything you write. You’re a fraudster. A pretender.
Sawa Mzee MS. Kubali kwa umri wako wewe ni sawa na chawa tu wa akina Sykes. Upo kichawa zaidi Mzee wangu, kwa hiyo familia. Huna lolote la maana unaloandika zaidi ya kuwasifia Sykes na kuendekeza udini.Schmidt,
Mimi sina tatizo na unavyoniona.
Hizi liberal inclined colleges and universities in the US huwa wanawaalika trending individuals kwenye fields mbalimbali toka dunia nzima wenye mitazamo mbadala ya ile iliyo rasmi kwenye seminars and lectures kwa manufaa ya wanafunzi wao, lakini haimaanishi wewe kualikwa huko North Western University kunakufanya uwe World Class Scholar. Hao Wanafunzi bado inabidi wachambue mbivu na mbichi. Hilo ndilo lengo lao hao Wazungu kukualika huko.Lokonga,
Katika maajabu niliyokutananayo ni hii historia ya Sykes.
Kila utakaemkuta katika historia ya Tanganyika yumo katika nyaraka zao.
Ajabu kubwa sana.
Unadhani nafanya utani?
Nimesoma barua za Chief Thomas Marealle katika nyaraka hizo.
Wanaelezana mambo makubwa ya hali ya baadae ya Tanganyika.
Bahati mbaya siwezi kueleza hayo kwa kuwa yalikuwa mazungumzo binafsi sana.
Unaumia kuwa kuna watu Allah aliwanyanyua kupita wengine.
Tungefahamu vipi historia ya Nyerere kama si nyaraka hizi za Sykes?
Nilialikwa Northwestern University Evanston Chicago kufanya mhadhara juu ya Abdul Sykes.
Hiki chuo ndiyo kinaongoza ulimwenguni katika African History.
Sikutegemea hata kwa mbali kama haya mambo yatakuwa makubwa kiasi hiki.
Yuko publisher aliposoma mswada wa kitabu cha Abdul Sykes aliniambia kuwa mswada wangu ni mgodi wa dhahabu.
Lakini aliogopa kuchapa kitabu changu.
Miaka hiyo mimi kijana kiasi miaka 30.
Samahani sana kama unatabishwa na kalamu yangu.
Kitabu kinakwenda toleo la tano.
View attachment 2119388
View attachment 2119390
Schmidt,Hizi liberal inclined colleges and universities in the US huwa wanawaalika trending individuals kwenye fields mbalimbali toka dunia nzima wenye mitazamo mbadala ya ile iliyo rasmi kwenye seminars and lectures kwa manufaa ya wanafunzi wao, lakini haimaanishi wewe kualikwa huko North Western University kunakufanya uwe World Class Scholar. Hao Wanafunzi bado inabidi wachambue mbivu na mbichi. Hilo ndilo lengo lao hao Wazungu kukualika huko.
Schmidt,Sawa Mzee MS. Kubali kwa umri wako wewe ni sawa na chawa tu wa akina Sykes. Upo kichawa zaidi Mzee wangu, kwa hiyo familia. Huna lolote la maana unaloandika zaidi ya kuwasifia Sykes na kuendekeza udini.
Historia ya wachaga itaandikwa na wachaga wenyeww na historia ya waswahili itaandikwa na waswahili wenyewe kila mtu aandike historia yake
Mdukuzi,Historia ya wachaga itaandikwa na wachaga wenyeww na historia ya waswahili itaandikwa na waswahili wenyewe kila mtu aandike historia yake
Kwahiyo unataka kusema hakupewa support na mamangi wengine maana juzi kutawazwa Samia Kilimanjaro tumeonyeshwa mamangi wengi Uchaggani! Sidhani kama mzee Kirama alikuwa na influence Uchaggani kote mbali na Machame! Na hata kama walikuwa wamenyongwa na Wajerumani ikumbukwe Wajerumani walikuwa Tanganyika mpaka 1918 tu na Waingereza walirudisha Umangi kupitia Chieftancy! BTW Wajerumani walinyonga Wamangi wote Uchaggani na around Tanganyika watemi na machifu!KUMBUKUMBU KIFO CHA MANGI MKUU THOMAS MAREALLE 14 FEBRUARY 2007: PARAMOUNT CHIEF THOMAS MAREALLE KATIKA NYARAKA ZA RAJABU IBRAHIM KIRAMA WA MACHAME NKUU
Mara yangu ya kwanza kusoma historia ya Mangi Mkuu Thomas Marealle ilikuwa ndani ya Nyaraka za Sykes wakati natafiti kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.
Kwa bahati mbaya sikuweza kutumia yale niliyosoma katika kitabu nilichokuja kuandika kwa kuwa mengi katika yale niliyosoma yaikuwa mambo binafsi zaidi kuliko historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ingawa jina la Nyerere lilikuwa likijitokeza.
Nimekuja kukutana tena na Mangi Mkuu Thomas Marealle baada ya kiasi cha miaka 30 kupita katika Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama wakati natafiti maisha ya Mzee Rajabu wa Machame Nkuu.
Napenda kama kumbukumbu ya kifo cha Mangi Mkuu nieleze machache katika yale ambayo nimejifunza katika kusoma barua walizokuwa wakiandikiana watu hawa wawili kutoka Kilimanjaro kila mmoja akiwa na nafasi muhimu katika jamii ya kabila la Wachagga.
Thomas Marealle akiwa kwanza Mangi wa Marangu kisha Mangi Mkuu wa Wachagga, Rajabu Kirama yeye akiwa kiongozi wa Waislam na mtu aliyeueneza Uislam Uchaggani akianzia harakati zake kijijini kwake Machame Nkuu katika miaka ya 1930.
Harakati hizi zilileta uadui mkubwa kati yake na Chief Shangali.
Mwishoni wa miaka ya 1800 Wajerumani baada ya kuchoshwa na vita visivyokwisha baina ya Wachagga wenyewe kwa wenyewe waliamua kuwakamata takriban mangi wote isipokuwa Shangali na Marealle.
Jumla ya mangi 19 walinyongwa hadharani isipokuwa Chief Marealle na Chief Shangali.
Haya ndiyo madhila yaliyowakumba Wachagga chini ya utawala wa Wajerumani.
Watoto wa machifu hawa wawili hata hivyo walikuja kupata nguvu kubwa sana katika utawala wa Waingereza.
Katika utawala wa Waingereza na katika hali ya amani na utawala Wachagga waliunda chama - Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU) (Umoja wa Raia wa Kilimanjaro).
Petro Njau akiwa kiongozi wa chama hiki alipewa jukumu la kusimamia maslahi ya Wachagga kama taifa.
Katika kanuni za KCCU kanuni hizi zinawataja Wachagga kama watu waliozaliwa huru na wenye haki ya kulinda uhuru wao.
Petro Njau alikinadi chama hiki kuwa ni ‘’chama cha siasa cha kikabila.’’
Nilipokuwa nasoma Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama nilishangaa sana kusoma kuwa Wachagga kwa asili waliichukulia Kilimanjaro yote kuwa ni nchi.
Nyaraka za KCCU zimejaa maneno ya itikadi ya: ‘’nchi,’’ ‘’taifa,’’ ‘’raia,’’ ‘’uchaguzi,’’ ‘’kura,’’ na ‘’utawala.’’
Petro Njau Rajabu na Ibrahim Kirama walikuwa wanaunganishwa na kukubaliana katika jambo moja kubwa na muhimu sana katika utawala wa Wachagga nalo ni kuwa Mangi walikuwa na nguvu zilizopea wakati raia wao hawakuwa na sauti yoyote.
Kwa ajili hii basi wanastahili kuondolewa wote na awekwe kiongozi mmoja tu atakaetawala Kilimanjaro yote na Wachagga wote.
Petro Njau alikuwa mwandishi wa Mzee Rajabu na pia mwandishi wa Chief Thomas Marealle pale Kilimanjaro ilipokuwa katika siasa za uchaguzi kutafuta Mangi Mkuu atakaekuwa juu ya Mangi wote, yaani Paramount Chief.
Rajabu Kirama alisimama bega kwa bega na Petro Njau katika fikra hii.
Thomas Marealle na Abdiel Shangali ndiyo walikuwa wanagombea nafasi ya Mangi Mkuu na bahati mbaya sana kwa Abdiel Shangali ni kuwa alikuwa na uadui mkubwa na Rajabu Ibrahim Kirama.
Rajabu Kirama akasimama kumsaidia Chief Marealle awe kiongozi wa Wachagga wote.
Hivi ndivyo Thomas Marealle alivyokuja kuchaguliwa kuwa Paramount Chief, yaani Mangi Mkuu.
Picha: Mzee Rajabu Ibrahim Kirama, Mangi Mkuu Thomas Marealle wa Marangu na Chief Abdiel Shangali wa Machame.
View attachment 2119338
Huyo chifu mpaka sasa amefanya wakibosho na wamachame hawaivani hata kuoleana,na suo hilo tuu hata nyumba mkibosho akijenga ni marufuku kugeuzia mlango usawa wa machame..
Nje ya mada;niliwahi ambiwa na mzee wangu kuwa huyu mariale haikuwa ukoo wake bali ni neno lilitokana na kupishana kauli baina ya mtu aliekuwa anamuulizia huyu mangi alikuwa amelala sasa akaja mzung kumtembelea sasa yule msaidizi wa chifu akamjibu (mangi nale))yaani kwa kichaga ni mangi kalala)sasa yule jamaa akasindwa kutamka lile neno akasemaa marialeee marialeeee ndio likawa chimbuko la kijiita jina hilo mariale mariale hadi likazoeleka.ila ukoo kabisa aliokuwa akitumia ni (mushi)
Sent using Jamii Forums mobile app
we mzee kila kitu ni sykes tuu
Who is shekhi Haruna?Schmidt,
Mimi nimesoma elimu ya mnakasha, yaani mijadala kwa Sheikh Haruna.
Huyu alikuwa mwalimu wa madrasa ambayo wewe umeiandika kwa dharau na kejeli.
Kanifunza mengi na mojawapo ni adabu.
Adabu akikusudia kuwa watu hawatukanani katika kujadili masomo ya kielm.
Sheikh Haruna alikuwa anasema ukiona mtu anakimbilia matusi jua ameshindwa na hapana haja ya kuendelea na yeye katika mjadala kwani matusi hayajibiwi.
Hana hqzinqMkuu unayo hazina ya historia, ila unachanganya na udini
Geza...kwahiyo unataka kusema hakupewa support na mamangi wengine maana juzi kutawazwa Samia Kilimanjaro tumeonyeshwa mamangi wengi Uchaggani! Sidhani kama mzee Kirama alikuwa na influence Uchaggani kote!
Ana taarifa taarifa fulani siyo mbaya sana, accumulated experienceHana hqzinq
Ana narrow steam ya anayotakq
A while ago nilimheshimu sana
Nikqjq kugundua ana verse moja tu