Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,009
- 60,629
Paranoia ni kitendo cha mtu kuwa na tabia ya kuwa na wasiwasi,hofu, shaka, na kutoamini mtu mwingine bila sababu ya msingi/ushahidi. Na mara nyingi hua inasukumwa na wivu uliopitiliza kiasi pia kukosa uelewa.
Inapotokea mmoja ya watu wawili ndani ya mahusiano anakua/act paranoid inapunguza amani ndani ya mahusiano, kunakua na tuhuma nyingi kumwelekea mtu ambae anaweza akawa hana hata mpango wa kufanya yale anayoshutumiwa ame/anafanya. Hali hiyo huweza kupelekea mahusiano yakavunjika hata kama mapenzi bado yapo kwasababu mtuhumiwa anachoka na anashindwa kujitetea kila siku na kwa kila jambo, na mwenzake kukosa uelewa.
Ndio pale unapokuta mtu anaquestion kila msg inayoingia kwa mwenzi wake, hata inayotoka kwa ndugu zake. Anaona kila aina ya kutendwa kwenye kila kitu. Mwenzake akila chakula kidogo, ametoka kula kwa hawara, mke akianza kupendeza/kujijali basi kuna mwanaume mwingine zaidi yake, jirani akiulizia "mama nanii hajambo" basi wana siri hao. Alimradi kila kitu kimeficha jambo nyuma yake na hata akieleweshwa hataki kuelewa.
Ukiwa na mtu ambae anaridhisha moyo na nafsi yako mheshimu kwa kumuamini mpaka pale atakapokupa sababu ya kuamini tofauti na hivyo pia jaribu/jitahidi kuwa muelewa pale unapoeleweshwa kitu ili kulinda mahusiano yenu. Usione vitu ambavyo havipo, usilazimishe matatizo wala usitafsiri vitu zaidi ya vilivyo. Mahusiano/ndoa zinatakiwa kuwapa watu furaha na sio kuwaondolea, jitahidi usiwe mmoja wa watu wanaowafanya wenzi wao watamani asubuhi isifike wala muda wa kurudi nyumbani toka kibaruani. Mfanye apende kuwa karibu yako na hamu ya kukurudia haraka iongezeke na sio ipungue kadiri siku zinavyokwenda.
A new fav quote from the movie WIFE vs SECRETARY. . . .make use of it.
"all the fighting and worrying people do, it always seems to be about one thing. They don't seem to trust each other. Well, I've found this out. DON'T LOOK FOR TROUBLE WHERE THERE ISN'T ANY, BECAUSE IF YOU DON'T FIND IT, YOU'LL MAKE IT.Just believe in someone.
Jumatatu njema!!