Paranoia. . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Paranoia ni kitendo cha mtu kuwa na tabia ya kuwa na wasiwasi,hofu, shaka, na kutoamini mtu mwingine bila sababu ya msingi/ushahidi. Na mara nyingi hua inasukumwa na wivu uliopitiliza kiasi pia kukosa uelewa.

Inapotokea mmoja ya watu wawili ndani ya mahusiano anakua/act paranoid inapunguza amani ndani ya mahusiano, kunakua na tuhuma nyingi kumwelekea mtu ambae anaweza akawa hana hata mpango wa kufanya yale anayoshutumiwa ame/anafanya. Hali hiyo huweza kupelekea mahusiano yakavunjika hata kama mapenzi bado yapo kwasababu mtuhumiwa anachoka na anashindwa kujitetea kila siku na kwa kila jambo, na mwenzake kukosa uelewa.

Ndio pale unapokuta mtu anaquestion kila msg inayoingia kwa mwenzi wake, hata inayotoka kwa ndugu zake. Anaona kila aina ya kutendwa kwenye kila kitu. Mwenzake akila chakula kidogo, ametoka kula kwa hawara, mke akianza kupendeza/kujijali basi kuna mwanaume mwingine zaidi yake, jirani akiulizia "mama nanii hajambo" basi wana siri hao. Alimradi kila kitu kimeficha jambo nyuma yake na hata akieleweshwa hataki kuelewa.

Ukiwa na mtu ambae anaridhisha moyo na nafsi yako mheshimu kwa kumuamini mpaka pale atakapokupa sababu ya kuamini tofauti na hivyo pia jaribu/jitahidi kuwa muelewa pale unapoeleweshwa kitu ili kulinda mahusiano yenu. Usione vitu ambavyo havipo, usilazimishe matatizo wala usitafsiri vitu zaidi ya vilivyo. Mahusiano/ndoa zinatakiwa kuwapa watu furaha na sio kuwaondolea, jitahidi usiwe mmoja wa watu wanaowafanya wenzi wao watamani asubuhi isifike wala muda wa kurudi nyumbani toka kibaruani. Mfanye apende kuwa karibu yako na hamu ya kukurudia haraka iongezeke na sio ipungue kadiri siku zinavyokwenda.

A new fav quote from the movie WIFE vs SECRETARY. . . .make use of it.
"all the fighting and worrying people do, it always seems to be about one thing. They don't seem to trust each other. Well, I've found this out. DON'T LOOK FOR TROUBLE WHERE THERE ISN'T ANY, BECAUSE IF YOU DON'T FIND IT, YOU'LL MAKE IT.Just believe in someone.

Jumatatu njema!!
 
Kabisa kabisa without TRUST a relationhip is doomed to fail....Hakuna anaye kataa hapo.

Afadhali afadhali leo umekuja na point nzuri sanai.
 
'DON'T LOOK FOR TROUBLE WHERE THERE ISN'T ANY, BECAUSE IF YOU DON'T FIND IT, YOU'LL MAKE IT.Just believe in someone.'


ni ngumu kumeza 'DONT LOOK'
mimi naona LOOK kimyakimya bila mwenzio kujua unalook, ukijiachia sana utajashtukia kuna mafuriko pindi UTAKAPOSHINDWA KUPUMUA maji yamekuzingira kitanda wewe ukiwa usingizini
 
Miss MariaAntonia tatizo lipo kwenye wewe kulazimisha makosa yawepo iwapo utayakosa. Just be careful. . .
 
mmh lkn ukiona 2 viredflag vina kuallert, ni bora kuchukua ha2a madhubuti la sivyo kweli kbs utakuta too late maji yamekufika shingoni.
ila asante kwa ujumbe mzuri lizzy.
 
Lizzy,nimependa sana hii kitu,
Na huwa inakuwa ni matokeo ya kutokubali kusahau historia ya matukio yaliyomtokea mtu siku za nyuma,
Na kujikuta unashindwa kumtofautisha mwenza wako na aliyekuumiza kabla yake na kuhusi wanaume wote/wanawake wote ni sawa au wananafanana,

Nashauri km tumeshaamua kuanza upya basi tufute historia zetu hasa za kuumizwa kwan huwa hatuwatendei haki wale wapya tulioanza nao na mwisho wa siku tunajikuta tunaishi maisha ya wacwac na tuhuma zisizoisha na mwisho wa siku nao wanachoka na kuamua kuanza mbele na kutuacha na vilio na kumsingizia shetan kumbe ni matatizo yetu wenyewe.
 
Dah, nakubaliana na Lizzy, paranoia inaharibu kabisa mahusiano.
Hasa pale ambapo paranoid kapenda.

Kila kitu kama unafanya, fanya kwa kiasi ukizidisha inakuwa tatizo.
Na hii inakuwa na atharui kubwa zaidi ambapo mwanamke anakuwa paranoid kwa mwanamme
Kama ujuavyo, mwanamme hapendi kuwa possesed, ukianza kum-possess tu anatimka na kuacha vumbi kama treni.

Lakini paranoia, lazima iwepo japo kidogo tu jamani, kosa hili ni kama la hausi gelo kula mboga jikoni halimfukuzishi kazi.lol
 
Paranoia ni ugonjwa wa akili kama yalivyo magonjwa mengine ya akili, mtu mwenye tatizo hili anahitaji msaada wa haraka wa tiba, maana itakuwa ni vigumu kwake si kujenga tu uhusiano imara na mwenzi wake bali pia hata jamii iliyomzunguka.
Naamini sio vibaya kumwambia mtu mwenye tabia hizo kuwa yu mgonjwa, na anahitaji tiba ya haraka, kwani huo utakuw ani msaada mkubwa sana kwake. wengi wetu hapa kuna watu waliotuzunguka, wanaweza kuwa ni wenzi wetu, marafiki zetu, wafanyakazi wenzetu au jamaa zetu wanaokabiliwa na tatizo hili, lakini tunaona haya kuwaambia ukweli kuwa ni wagonjwa. Hata kama wakitukasirikia, lakini tutakuwa tumewasaidia sana katika maisha yao ya kimahusiano.

Ahsante sana Lizzy kwa kulizungumzia hili. kwani wengi tumekuwa tulileta mada humu za watu wenye tatizo hili lakini tumekuwa tukizunguuuka wakati ukweli ndio huu.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa kuna watu wana 0% ya paranoia?

 
mwanaume anatakiwa aishi kiuanaume
na sifa kubwa ya mwanaume anatakiwa awe na confidence
mi maswali kama.ulikuwa wapi? nani kapiga simu? yule kwenye picha nani? na maugovi ya wivuwivu kwenye mahusiano na malawama yasiyo na sababu siwezi kuvumilia
hapo lazima red card itembee
mtu akiamua kuwa mbaya kwenye mahusiano anakuwa tu.ni ngumu kujua especially na hzi teknologia
SO CONFIDENCE NA UHUSIANO NI KITU MUHIMU SANA
NAOMBA MSINIJADILI
:focus:
 
Lizzy,

Haya mambo siyo rahisi hata kidogo,

It all begins and ends with you, only you......!!

Kwani kama wewe mwenyewe ni mwizi bazi lazima utakuwa na hisia kwamba na wewe pia unaibiwa!!

Hatua za kuchukua baada ya hapo ndio tunakuwa mbayu wayu!!

Babu DC!
 
Kwanza za asubuhi, mimi ningekuomba japo unipe hints due early stage diagnosis of that disease !
 
Ka ukweli kapo kabisaaa hapo....wakati mwingine huwa tunasahau kuwa 'ukimchunguza sana bata hutamla'...japokuwa yupo bandani kwako.
 
Hayo ni maradhi ya kimalezi,yanatibika kwa ushauri,tatizo mtu mwenye maradhi haya hajui kama anayo mpaka akutane na mtaalamu wa saikolojia!So ushauri kwa hawa ni kuwakutanisha na madaktari hawa wa saikolojia!
 
Hayo ni maradhi ya kimalezi,yanatibika kwa ushauri,tatizo mtu mwenye maradhi haya hajui kama anayo mpaka akutane na mtaalamu wa saikolojia!So ushauri kwa hawa ni kuwakutanisha na madaktari hawa wa saikolojia!

Samahani sana ndugu,

Kwani huo ugonjwa una level moja tu? Hakuna wale ambao hali yao ni mild na wale ambao ni serious?
 
Babu DC,nakusalimu!Nijuavyo mimi haya ni maradhi yanayotokana na malezi kwa kias kikubwa,so inafikia ugonjwa unaonekana ni mtu anaingia kwenye ndoa so ni ukubwani,muda unakua umepita,hivyo lazima anakua tayari ni siriaz,kuepusha hali ya kuwa siriaz ni kumuwahi mtu akiwa kwenye familia kwa kubadili malezi!
 
Nakubaliana na wewe Babu DC

Ndo maana nikasema paranoia nayo inategemea ni kiasi gani

Kama ni kupima in % unaweza kuta mtu ana 10% lakini haijaanza kuleta madhara makubwa
Na mwingine unakuta ni 90% ambayo haivumiliki


But to some extent, watu wengi ni paranoia kwa level fulani
Ndo maana ukimkuta mpenzi wako anatoka guest
Lazima uulize ni nini kinendelea hapo hasa kama hakukuambia atapita huko
Lakini je kukutwa unatokea mlango wa guest ni kwamba unacheat?

Samahani sana ndugu,

Kwani huo ugonjwa una level moja tu? Hakuna wale ambao hali yao ni mild na wale ambao ni serious?
 

Bado kidogo ndugu, usichoke kunisaidia. Inaanziaje kwenye familia alikolelewa na kukulia mtu? Yaani anaanza kuwa paranoiac kwa wazazi wake na majirani au??
 

Kweli dada mkuu,

Katika hii dunia, kila mtu ana level fulani ya ukichaa ila kuna wale ambao wamepitiliza na kuwa machizi kabisa!!

Babu DC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…