Achilia mbali goli lolote, PSG wamekuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kutawala mchezo katika hatua ya makundi, wakiwa wameigaragaza Bayern Munich, Anderlecht na Celtic, timu nyingine za Kundi B. Wameshinda kila mechi kwa angalau magoli matatu.
Celtic wamepata kipigo kizito kwa kufungwa 12-1 katika mechi mbili, na wamekuwa vibonde wa PSG walioshinda kwa kishindo Ligi ya Mabingwa Jumatano.
Hata hivyo, licha ya umahiri wao katika kumiliki mchezo, PSG bado hawajamaliza kazi kwenye kundi lao. Bayern Munich wapo nyuma yao kwa pointi tatu na timu hizo zinatarajiwa kukutana kwenye mechi ya mwisho hatua ya makundi Disemba 5. Bayern wanataka kulipa kisasi cha kipigo cha 3-0 Parc des Princes, ikiwa wataweza kuibuka na ushindi wa mabao manne, watafaanikiwa kuipiku PSG na kukaa kileleni mwa kundi.