msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Baada ya kuangazia makundi ya watu wanaochukia utawala wa Rais Samia sasa ni zamu ya makundi yanayoridhishwa ama kufurahishwa na utawala wake.
1. WAFANYABIASHARA
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wamepita kwenye dhoruba na sekeseke zito katika biashara zao ikiwemo kubambikiwa kodi, kutishiwa ama kushitakiwa kwa kesi za uhujumu uchumi, kufungiwa biashara zao na hata wengine kutekwa na watu wasiojulikana.
Baada ya ujio wa Rais Samia tumeona ama kushuhudia wafanyabiashara wakipata ahueni katika biashara zao ambapo baadhi kwa waliokuwa wamefunga wameanza kufungua biashara zao, waliokuwa wanaogopa kuwekeza kwenye biashara kwa sasa wameanza kuwekeza, vilio vya wafanyabiashara kuchukuliwa pesa kwenye akaunti zao kinyume na makubaliano kwa sasa havisikiki tena.
Hivyo kiujumla kwa sasa wafanyabiashara ni miongoni mwa watu watakaofurahia utawala wa sasa kulinganisha na uliopita kwani Rais Samia kaanza kuwatengenezea mazingira rafiki ya kufanya biashara zao kwa uhuru licha ya changamoto za hapa na pale ikiwemo ya kuwapanga wafanyabiashara wadogo almaarufu kama 'machinga'.
2. WATUMISHI WA UMMA
Ni miongoni mwa wahanga wa utawala uliopita kwani katika kipindi chote cha miaka mitano mfululizo wamenyimwa haki zao za kiutumishi ikiwemo kupandishwa vyeo na madaraja. Hivyo kwa ujio wa Rais Samia wamekuwa na matumaini mapya kwani haki zao za msingi walizozikosa kwa muda mrefu zimeanza kufanyiwa kazi huku sikio lao wakizidi kulitega kwenye mei mosi ya mwakani ambapo mama Samia anaenda kuwarejeshea furaha yao waliokosa kwa kipindi kirefu.
3. VIJANA WASOMI WASIO NA AJIRA
Huwezi kutaja wahanga wakubwa wa awamu ya tano bila kuwaweka vijana wa kundi hili. Kwani ni katika awamu ya tano ambapo tumeshuhudia vijana hawa wakidharualiwa na kukejeliwa wazi wazi na baadhi ya waliokuwa viongozi wa utawala uliopita ikiwemo kuambiwa kuwa wajiajiri ingali hawana mitaji ya kujiajiri kwa chochote.
Hivyo basi, baada ya mh. Samia kuingia madarakani kundi hili limekuwa na matumaini mapya kwamba huenda 'chief hangaya ' akawafuta machozi kwa kutoa vibali vya ajira tofauti na aliyekuwa mtangulizi wake ambaye yeye 'ajira kwa vijana' hakikuwa kipaumbele chake. Ingawa kundi hili linaweza kubadili uelekeo endapo fursa za ajira zitaendelea kubanwa kama ilivyokuwa katika awamu iliyopita.
4. WAPAMBANAJI NA WACHAKARIKAJI
Hawa wana malengo ya kufika mbali na kufanikiwa kimaisha hivyo wanaamini ndoto zao zitatimia kupitia uwepo wa utawala bora unaojali haki za binadamu chini ya chief Hangaya na sio ubabe na ukatili kama ilivyokuwa katiaka utawala wa mwendazake.
5. WAHANGA WA SIASA ZA DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA
Hapa nazungumzia baadhi ya wanasiasa waliokuwa wahanga wa siasa za mwendazake hususani wa kutoka vyama pinzani kwa sasa wana auheni ya kushiriki siasa za kukosoa mwenendo wa serikali licha ya changamoto za hapa na pale ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi na kuhakikisha kwamba suala zima la utawala bora na demokrasia vinarejeshwa katika hali yake. Kwa kifupi kundi hili kwa sasa linapumua kulinganisha na mateso na manyanyaso waliopitia katika utawala na siasa za mwendazake.
Hata hivyo makundi ya watu wanaomkubali chief Hangaya ni mengi ila kwa sababu ya muda nimeona niainishe hayo machache yaliyoguswa moja kwa moja na utawala uliopita na hivyo naishia hapa kwa siku ya leo.
Pia soma,
Thread 'PART 1: Hawa hapa watu wanaomchukia na kuchukia utawala wa Rais Samia' PART 1: Hawa hapa watu wanaomchukia na kuchukia utawala wa Rais Samia