Pascal Mayalla ataka wataalamu wa Kemia waje watueleze sintofahamu ya Fumigation na Barakoa baada ya kutafakari hotuba ya Rais Magufuli

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mwandishi wa habari nguli mh Pascal Mayalla amewataka wataalamu wa Kemia kuja hadharani na kutuchambulia faida na hasara za kupiga fumigation mitaani na kwenye vyombo vya usafiri kama kuna tija kwenye mapambano dhidi ya Corona.

Kadhari watuelimishe juu ya ubora wa barakoa kama zinaweza kuttumika kuihujumu nchi kwa kuletwa zikiwa na vimelea vya Corona.

Pascal na Dotto Bulendu wamesisitiza kuwa huu sio wakati wa kuwaachia waandishi wa habari waliosoma HGL na HGK pekee kuripoti habari za Corona bali wanahitajika wabobezi wa maswala ya afya katika kulihabarisha taifa.

Chanzo: Star tv
 
Kama maagizo yashatamkwa kutoka juu...

Wataalam wa kemia wao ni wakina nani wakuja na hoja za kupingana na maagizo yaliyotoka juu...

Cc: mahondaw
 
Mwandishi wa habari nguli mh Pascal Mayalla amewataka wataalamu wa Kemia kuja hadharani na kutuchambulia faida na hasara za kupiga fumigation mitaani na kwenye vyombo vya usafiri kama kuna tija kwenye mapambano dhidi ya Corona.

Kadhari watuelimishe juu ya ubora wa barakoa kama zinaweza kuttumika kuihujumu nchi kwa kuletwa zikiwa na vimelea vya Corona.

Pascal na Dotto Bulendu wamesisitiza kuwa huu sio wakati wa kuwaachia waandishi wa habari waliosoma HGL na HGK pekee kuripoti habari za Corona bali wanahitajika wabobezi wa maswala ya afya katika kulihabarisha taifa.

Source Star tv
Msihangaike lengo la jamaa ilikuwa ni kuwaingiza wanyonge Chaka ili wasiitake serikali hii inayonuka madeni na ufukara kuweka ruzuku kwenye mask bora
 
Bongo hatuheshimiani kwa taaluma, hao unaowaita wandishi wa habari wapo kwenye vyombo vya kueneza habari... lakini cha ajabu hawajisumbui kuwahoji wataalamu.

Kila saa mahojiano na wasanii, eti watu maarufu... ona hadi matangazo ya kuelimisha watu kuhusu kujihadhari na Corona wapo Snura na Sholo Mwamba sijui Gigi Money 🤷🏾‍♂️

Hao wataalamu watasikika kupitia wapi.?

Huyo Pascal Mayalla atuambie ni lini amealika na kuhoji Wakemia kwenye vipindi vyake.
 
Back
Top Bottom