lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Watu waliomjua Pascal Kupitia JF pekee poleni sana. Huyu jamaa hanijui lakini Mimi namjua sana.
Watanzania wengi twamjua sana, EAC wengi wanamjua sana ingawa yeye anawajua kwa kuwaona watu wachache sana lakini mamilioni ya watu tunamjua.
Kwa sababu gani?
Kwa sababu ni mtu mtangazaji marufu Sana hapa Tanzania.
Umaarufu wake ulisababishwa na nini?
Kwa wasiokua historians huyu ndo mwanzilishi wa jina maarufu lililo hai hadi leo la “KITI MOTO.”
Neno kiti moto leo hii linatumika kama hivi, “Leo nyumbani nimewekwa kiti moto na wazee kwanini sitaki kuoa" au "Yule mtu leo kawekwa kiti moto hadi kalipa deni lake"
Lakini kubwa kuliko yote jina Hilo likaitwa kwa hivi, "twendeni nikawanunulie kiti moto pale wanajua sana kuitengeneza nyama ya kiti moto”
Mwanzilishi wa jina au msemo huo maarufu ni Pascal Mayala.
Umaarufu wake ni huu.
Kwa kifupi miaka ya 1995 hivi kama sijakosea Pascal alianzisha kipindi kilichopendwa na kutazamwa na Watanzania wengi sana na hata wasio Watanzania.
Kipindi hiki ilikuwa ukikikosa unajuta, maofisini, mitaani, magengeni, mabaa mahospitalini na maeneo mengine mazungumzo yalikuwa ni juu ya kipindi cha jana usiku cha kiti moto.
Kiti moto ilikuwa inaita watu maarufu hususan viongozi na Pascal alikuwa anawauliza masuali ambayo kwa kweli walikuwa wanaona kiti kinaunguza.
Hata kiongozi ajitetee vipi dogo Pascal atambana tu hadi mhojiwa atapoteza mwelekeo.
Pascal alihoji maswali tata sana hadi wewe mtazamaji unaanza kumuonea huruma muulizwa.
Kwa ufupi kilikuwa kipindi kitamu sana na watu makini hawakupenda kukosa kukiona. Maswali yake yalikuwa mazuri, ya msingi, ya kujenga ingawa wakuu walikiona cha Moto kweli.
Huyu Pascal wa JF sio yule, najua kazeeka yule alikuwa Bomba akiwepo kwenye press live akipewa nafasi ya kuuliza swali watazamaji wote utulivu ili kumsikiliza.
Huyu wa JF kazeeka. Ameamua kukubalika kutukanwa mitandaoni kisa anatoa mada ngumu kuzielewa kwa vijana wa leo. Mada za mafumbo, za kuuma na kupuliza, za kutotaka lawama, anaishia kutukanwa na madogo.
Yeye ukimlaumu atakuambia
"Read between the lines"