Pascal Mayalla kazeeka haoni mbele

Ben saa8 ni kesi ya mbowe hiyo ...sijui kwanini watu awaamini kuwa ni kesi ya mbowe ...hivyo mnaotaka kujua alipo ben basi mkamateni mbowe mminyeni puuumb atawaambieni alipo mzika wapi, hapo mimi nasema wazi japo ccm ni mavii tu ila kwenye swala la ben naitoa ccm.
 
Nasikia Mbowe pia ndio alimmimiminia risasi Lissu.
 
Nimependa majibu yako mkuu P. Mayalla. You are not negatively biased!
 
Mkuu lee van cliff , kwanza asante tena kunianziashia thread
Tumuombee mwanaJF Pascal Mayalla apitishwe

Wote tuseme Amen!
Mkuu Yahana Mbatizaji, johnthebaptist , amen, amen!.
Hili jambo nimelianzia hapa
Nikakumbana na Kikwazo cha kwanza hapa Licha ya vikwazo kadhaa, hatimaye nimefanikiwa kuianza ile safari. Asanteni kwa sala zenu zimesaidia ila bado zinahitajika sana! Mungu nisaidie
Nikatoa ushauri kwa chama changu kuhusu EALA Ubunge EALA, Wito Kwa CCM, Msiangalie Ukwasi, Tuteulieni, Wazalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Wenye Uwezo na Uzoefu wa Kimataifa Kutuwakilisha Ipasavyo
Kazi ya Uelimishaji Umma kuhusu EAC inaendelea Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Fursa za Mtangamano
Tukaitwa Dodoma kuhojiwa, huko nikakutana na A shock of my life, furaha yageuka shubiri. Be good to people on your way up, you might meet them on your way down, mwenzenu leo yamenikuta!
Sasa leo ndio kikao cha CC kuchuja majina, hivyo sala zenu zinahitajika sana kuliko wakati mwingine wowote!.
Mungu Nisaidie!.
P
 
Kazi iendelee
Wanabodi, kwenye bandiko hili Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... nilishauri
Hata baada ya kuteuliwa kuwa Mwenezi wa CCM, Paul Makonda bado anapigwa vita na wasiomtakia mema, wasioitakia mema CCM na wasio itakia mema Tanzania.

Japo Tanzania ni nchi ya vyama vingi, na kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mamlaka kuu ya nchi ni wananchi, kupitia katiba, serikali ya CCM ilifanya mabadiliko ya katiba kinyume cha katiba na kupoka ukuu wa mamlaka kuu ya wananchi, na kuikakabidhi kwa chama cha siasa, ambapo sasa mamlaka Kuu ya nchi ni chama tawala, CCM ndio imeshika hatamu kuongoza serikali, hivyo katika ukuu wa chama, CCM ndio kila kitu, hivyo Makonda kama msemaji wa CCM, kikao cha CCM kinaweza kumwagiza Rais wa JMT atekeleze jambo lolote lililoelekezwa kwenye ilani ya CCM, Katibu Mwenezi ndie msimamizi wa ilani ya CCM, ana mamlaka yote ya kumuamrisha hadi Rais wa JMT, atekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo Makonda yuko very right kumuamrisha Waziri Mkuu na kumpa ultimatum ya miezi 6 kumaliza migogoro yote ya ardhi ya nchi hii.

Na baada ya miezi 6, kama Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa atashindwa kuitatua migogoro yote ya ardhi, atakuwa ni ameshindwa kazi, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, itakutana na kumuagiza Rais wa JMT, kumuondoa Waziri Mkuu, kwa kushindwa kazi na kumteua Waziri Mkuu mwingine mwenye uwezo.

Hata ikitokea Rais Samia ameshindwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, chama kinaweza kumfuta uanachama na hivyo kupoteza urais!, hivyo Mwenezi wa CCM ni mtu mkubwa sana, kuliko serikali yote ya Tanzania, na hii ndio maana halisi ya Party Supremacy, CCM ndio imeshika hatamu za kuiongoza serikali ya Tanzania .

Hongera sana Mwenezi mpya wa CCM, Paul Makonda, kuiheshimisha CCM, endelea kutoa maagizo na ultimatum kwa viongozi wote kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, wewe ndiye msimamizi wa ilani ya CCM!.

Angalia ilani ya CCM imeelekeza nini kuhusu Bunge la JMT, toa maelekezo kwa Spika with ultimatums, Spika akishindwa kutekeleza Spika anaondolewa!, enzi za Spika Sitta, aliponea chupu chupu kuondolewa, kuna mtu mmoja very powerful ndani ya CCM aitwae "The King Maker" ndie alimuokoa Spika Sitta kwa kumpa maelekezo Mwenyekiti wa CCM, JK, na hii ndio salama yake!.

Makonda angalia ilani ya uchaguzi ya CCM inasema nini kuhusu mhimili wa Mahakama, toa maagizo with ultimatum kwa Jaji Mkuu atekeleze.

Angalia ilani ya uchaguzi inasema nini kuhusu majeshi, ulinzi na usalama, toa maelekezo with ultimatum kwa Amiri jeshi Mkuu na kwa Mkuu wa majeshi, IGP , etc.

Ila kwa nafasi ambazo sio za kichama kama Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi, CAG, Mwenyekiti wa NEC, Msajili wa Vyama vya Siasa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi, Mwenyekiti wa Tume ya Utawala Bora na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma ambao ni wateule wa rais, Paul Makonda anaweza kuwapa maelekezo bila ultimatums kwasababu hawa chama hakiwezi kuwafanya chochote, na badala yake, chama kitampa maelekezo mamlaka yake ya uteuzi ambaye ni Rais wa JMT, awaondoe!.

Kiukweli ninamkubali sana Paul Makonda!, Tangu nilipoanza kumkubali Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
He has never let me down!. Tena niliwahi kushauri Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... ushauri huu still stands, kwasababu miaka hii 4 ya Mama ni kumalizia awamu ya Magufuli, awamu ya baada ya Magufuli inaanza 2025, ila Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke hivyo you never know with politics, everything is possible!.

Paul Makonda kanyaga mwendo, chapa kazi, kazi iendelee!.
Paskali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…