Pasha: Mnanikosea heshima kunishindanisha na Harmonize

Pasha: Mnanikosea heshima kunishindanisha na Harmonize

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
BURUDANI Mnanikosea heshima kunishindanisha na Harmonize.

Hapo jana Msanii Pasha Mtepa akifanya Mahojiano na kituo cha Runinga cha East Afrika TV alisema watu wanamkosea heshima kumshindanisha na Harmonize kwa sababu yeye ndio wa kwanza kuuwakilisha mkoa wa Mtwara na amekaa muda mrefu kwenye game.

Pasha anasema wasanii wote wanaowakilisha mkoa wa Mtwara wanafanya vizuri kuanzia Harmonize, Ibraah na Kinata MC ila hataki kushindanishwa na Harmonize.

"Unanikosea heshima kunishindanisha na Harmonize, mimi nimefanya vikubwa sana nimekaa miaka 7 bila ngoma kabla yeye hajatokea lakini nimeishika mioyo ya wana Mtwara, nimewaheshimisha na wanajivunia kuhusu mimi" amesema Pasha.
 
Pasha anauza nguo pale Buza kanisani, kulinganishwa na Harmonize sio kosa bali wao wanapaswa kua pamoja
 
Hawa ndiyo maana wanahitaji kua na PR.

Jibu lake linalenga kumaanisha yeye ni big deal while angeweza lenga lionyeshe yeye na mmakonde mwenzake wanaitetea Mtwara so siyo sahihi kuwapambanisha.
Yeye anakataa eti ni level ingine.
 
Anasema Tu ili kufanya mambo yasiwe mengi,na vile Mtwara ni maarufu zaidi ya lindi,lkn ni wa Lindi kabisa
Anha hapo nimekuelewa.
Pia nimejaribu kurejea kwa mfano wanii wa Shinyanga wanaweza sema wao wa Mwanza.
 
Back
Top Bottom