Pasipoti, viza sasa kulipiwa benki

Pasipoti, viza sasa kulipiwa benki

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Pasipoti, viza sasa kulipiwa benki
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,December 22, 2008 @21:15

Idara ya Uhamiaji nchini imeanzisha utaratibu mpya ambapo kuanzia mwezi ujao, malipo ya huduma mbalimbali kama vile viza, pasipoti na vibali vya kuishi nchini, yatalipwa kupitia matawi ya Benki ya NMB.

Kamishna Mkuu wa Idara hiyo, Kinemo Kihomano alitangaza utaratibu huo mpya jana kwa waandishi wa habari Dar es Salaam katika taarifa yake iliyosomwa na Kamishna wa Pasipoti, Cuthbeth Sambalyegula.

Kihomano alisema utaratibu huo mpya utatumika katika Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Dar es Salaam, ofisi zote za mikoa na wilaya na baadhi ya vituo vya kutoka na kuingia nchini kama vile Namanga, Tarakea na Tunduma.

Alisema lengo la mabadiliko hayo ni kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato ya serikali ili kuhakikisha mapato hayo yanazidi kuongezeka. Alisema ingawa mapato yamekuwa yakiongezeka kila mwaka kwa kati ya asilimia 20 hadi 30, lakini kuna uwezekano wa mapato hayo kuongezeka zaidi.

Alisema lengo lingine ni kuongeza usalama wa fedha hizo kwani zinaweza kuibwa na majambazi wakati wa kusafirisha kama utaratibu huu wa sasa ukiendelea. Alisema utaratibu huo mpya pia utasaidia kupunguza msongamano kwenye ofisi za Idara hiyo kutokana na ufinyu wa nafasi kwenye ofisi hizo.

“Kwa utaratibu huo, wateja wa huduma za uhamiaji tunawasihi kulipia kupitia benki moja kwa moja badala ya utaratibu wa sasa ambapo huwa na adha kadhaa ikiwamo ufinyu wa ofisi zetu,” alisema Kamishna Mkuu huyo.

Alisema idara hiyo imeshafanya mazungumzo na kufikia makubaliano na Benki ya NMB na benki hiyo imekubali kutenga dawati maalumu kwa ajili ya wateja wa uhamiaji ili kuepusha adha ya msongamano. Alisema walichagua benki hiyo kwa sababu ina matawi mengi nchini hasa katika mikoa na wilaya ambazo idara hiyo inatoa huduma.

Kwa mujibu wa Mhasibu wa Idara hiyo, David Mbwilo, wafanyakazi wa idara hiyo ambao kazi zao sasa zitafanywa na benki, hawataachishwa kazi kwa kuwa idara hiyo ina uhaba wa wafanyakazi hivyo watahamishiwa vituo vingine vya kazi. Mbwilo alisema makusanyo ya fedha kwa mwaka jana yalifikia Sh bilioni 16.6 na mwaka huu ilikuwa inatarajia kukusanya Sh bilioni 20.4.
 
Hii nchi ya kitoto kweli ati hiyo nayo ni issue kubwaaaaa ya kupigia makelele mimi sijui kwa nini hilo suala limechelewa kiasi hicho!
 
its a good Move Uhamiaji....Yapo mengi mnaweza kuboresha...na kuzifanya Idara zingine kuamka...Hata kama imechelewa...it doesnt matter...Sie tunachohitaji ni kuboresha Huduma.

Wazo Langu kwa Uhamiaji: Nashauri pia Kila document hapo isafirishwe kwa Njia ya POSTA. Hapa mtaongeza Biashara ya Posta lakini pia itapunguza msongamano hapo wakati wa kuja kupokea passport au VIBALI vingine. Pia watu watapunguza RUHUSA kila wakati maofisini....Maana hapa bongo kila siku wafanyakazi wanaomba ruhusa...lkn wanahitaji kuongezwa mishahara!!!!

Lazima tukubali Shirika la POSTA linahitaji Kuboreshwa...Wenyewe POSTA wavivu kufikiria...wataanza kulalamika shirika likichukuliwa na Wawekezaji!!!
 
longo longo sasa hii...NMB yenyewe kwa foleni hawajambo
 
Alisema idara hiyo imeshafanya mazungumzo na kufikia makubaliano na Benki ya NMB na benki hiyo imekubali kutenga dawati maalumu kwa ajili ya wateja wa uhamiaji ili kuepusha adha ya msongamano.

Move nzuri, lakini hili la dawati maalumu litaongeza msongamano mara 100!!!
 
Press conference ni sawa kwa habari kuwafikia wananchi kwa haraka zaidi,ni hatua nzuri hiyo kwa uhamiaji kuamua hivyo lakini,wasiwasi wangu sijui kama lengo la kuboresha huduma litakuwa limefikiwa kupitia NMB!!Kwasababu,hilo dawati na hisi litalemewa na kusababisha foleni katika baadhi ya sehemu(miji/wilaya).
Binafsi kabla ya ku-launch nchi nzima,ingekuwa busara kama wangefanya kwanza pilot study kama inalipa with/without modifications then unapeleka countrywide.
 
its a good Move Uhamiaji....Yapo mengi mnaweza kuboresha...na kuzifanya Idara zingine kuamka...Hata kama imechelewa...it doesnt matter...Sie tunachohitaji ni kuboresha Huduma.

Wazo Langu kwa Uhamiaji: Nashauri pia Kila document hapo isafirishwe kwa Njia ya POSTA. Hapa mtaongeza Biashara ya Posta lakini pia itapunguza msongamano hapo wakati wa kuja kupokea passport au VIBALI vingine. Pia watu watapunguza RUHUSA kila wakati maofisini....Maana hapa bongo kila siku wafanyakazi wanaomba ruhusa...lkn wanahitaji kuongezwa mishahara!!!!

Lazima tukubali Shirika la POSTA linahitaji Kuboreshwa...Wenyewe POSTA wavivu kufikiria...wataanza kulalamika shirika likichukuliwa na Wawekezaji!!!

Ila huko NMB foleni yake mwanangu utalia maana huyo mfanyakazi itabidi aage kazini si chini ya masaa manne hadi sita.
 
Hii nchi ya kitoto kweli ati hiyo nayo ni issue kubwaaaaa ya kupigia makelele mimi sijui kwa nini hilo suala limechelewa kiasi hicho!

Kasheshe ubovu wa Nchi hii umeugundua lini mbona unaanza madongo kabla jogoo hajawika ?
 
Hapa hakuna chochote cha maana zaidi ya "Marketing Manager wa NMB" kufanya lobbying na watendaji wa idara ili kuhakikisha wanakuza biashara yao. Hapo usije kuta kuna extra charges kwa walipaji " Administrative fee" aka hela ya stationary na pango la benchi maalum.

Kwa nini hao uhamiaji wasiwe na account ya makusanyo Bank zote, kama CRDB, Stanchart, NBC, etc ili iwe rahisi kwa wateja wa Bank hizo kufanya transfer in one door na kupuwapunguzia na wao uwezekano wa kuibiwa wakiwa wametoa CASH Bank nyingine na kuelekea NMB kulipa? na hivyo kupunguza uwezekano wa foleni ya kufa mtu NMB?.
 
Pasipoti, viza sasa kulipiwa benki
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,December 22, 2008 @21:15

Idara ya Uhamiaji nchini imeanzisha utaratibu mpya ambapo kuanzia mwezi ujao, malipo ya huduma mbalimbali kama vile viza, pasipoti na vibali vya kuishi nchini, yatalipwa kupitia matawi ya Benki ya NMB.
ngrrrrrrrr ule msululu wa walimu wakipokea mshahara changanya na huu wa kuomba makaratasi mbona treni kibao.
 
Ni uamuzi mzuri lakini ni uamuzi ambao umechelewa sana, na bado kuna sehemu nyingi tu wanatakiwa wafuate utaratibu kama huo. Lakini wakumbuke kuwa NMB ni moja kati ya Benki ambazo ni dhaifu sana ki-utendaji na zinaendeshwa kwa mtindo wa kizamani sana. Ajabu mpaka leo bado kuna misururu na urasimu wa kijingkijinga. Kama TRA nao wangefuata utaratibu kama huu nadhani mambo ya rushwa yangepungua sana....
 
Uhamiaji kuamua kutumia Bank kwa ajili ya makusanyo ya pesa ni jambo jema sana. Maana tusingekawia kusikia "pesa kiasi kadhaa kimeibiwa Uhamiaji na wafanyakazi kadhaa wanashikiliwa na Polisi". Imeshatokea kwenye taasisi zisizotumia ujanja huu. Pongezi kubwa kwa Uhamiaji kwa hatua mnayoamua kuichukua.

Mara zote, haijawahi kuwa vibaya kugundua makosa na kuchukua hatua za haraka kusahihisha kabla balaa halijatokea. Tusiwe wachoyo wa pongezi. HII NI HATUA NJEMA.
 
Ni uamuzi mzuri lakini ni uamuzi ambao umechelewa sana, na bado kuna sehemu nyingi tu wanatakiwa wafuate utaratibu kama huo. Lakini wakumbuke kuwa NMB ni moja kati ya Benki ambazo ni dhaifu sana ki-utendaji na zinaendeshwa kwa mtindo wa kizamani sana. Ajabu mpaka leo bado kuna misururu na urasimu wa kijingkijinga. Kama TRA nao wangefuata utaratibu kama huu nadhani mambo ya rushwa yangepungua sana....

Mkuu mbona TRA wao wanakautaratibu huu siku nyingi tu? Nadhani uhamiaji na idara nyingine nyingi za serikali walijisahau sana.
Harafu hii NMB kwa foleni nadhani uhamiaji wameanzisha shida nyingine tu. Hilo benchi kama NMB wameshindwa kuwasaidia waalimu hapo si ndio tuseme kila kitu walishashindwa na hata hili wanaita benchi ni uongo wa kibiashara tu? Sisi watanzania tunakubali kila aina ya mateso tu jamani. Haya basi.
 
its a good Move Uhamiaji....Yapo mengi mnaweza kuboresha...na kuzifanya Idara zingine kuamka...Hata kama imechelewa...it doesnt matter...Sie tunachohitaji ni kuboresha Huduma.

Wazo Langu kwa Uhamiaji: Nashauri pia Kila document hapo isafirishwe kwa Njia ya POSTA. Hapa mtaongeza Biashara ya Posta lakini pia itapunguza msongamano hapo wakati wa kuja kupokea passport au VIBALI vingine. Pia watu watapunguza RUHUSA kila wakati maofisini....Maana hapa bongo kila siku wafanyakazi wanaomba ruhusa...lkn wanahitaji kuongezwa mishahara!!!!

Lazima tukubali Shirika la POSTA linahitaji Kuboreshwa...Wenyewe POSTA wavivu kufikiria...wataanza kulalamika shirika likichukuliwa na Wawekezaji!!!

sasa sikilizia hiyo foleni hapo bank..... kuchukua tu hela toka CASH POINT NI ISHU
 
Back
Top Bottom