deezekiels
Member
- Mar 20, 2014
- 42
- 3
Habarini wana jf, naomba mawazo yenu ya khari na mali kuhusu changamoto hii ya ombi la pasipoti, kwani dhumuni langu la kuomba pasipoti ni kujisajiri katika international english language testing system na baada ya kupata cheti hicho natarajia kuomba online scholarship ambazo kiukweli zinapatikana kwenye mitandao, lakini baada ya kusoma fomu za maombi na kuonana na ofisa wa uhamiaji imeonekana kwamba pasipoti inatolewa hasa kwa madhumuni ya safari za nje ya nchi kwa malengo tofauti mfano; ajira, michezo, masomo, dini, mialiko n.k tena uwe na vithibitisho vya safari husika. je kwa lengo hili la kujiunga na IELTS na baadae niombe online scholarship nitumie sababu au madhuni yapi au nitumie njia gani???