Passport ya Pharaoh (Ramesses 2)

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,774
Reaction score
47,866
Baada ya kugundulika mwili wa Pharaoh Ramesses 2 katika makabuli ya wafalme (Valley of Kings) huko Misri Rais wa Ufaransa Valéry Giscard d'Estaing katika miaka ya 1980 alifanikiwa kuishauri serikali ya Misri ikubali ombi lake la kuupeleka Mwili wa pharaoh huko Ufaransa ili ukafanyiwe preservation dhidi ya wadudu na hatari nyingine ambazo zingeweza kuuathiri mwili huo.

Serikali ya Misri iliamua kutoa passport kwa ajili ya Pharaoh ambaye alikuwa ameshafariki mwaka 1213 BC, katika passport hiyo ili kuonesha heshima kwa pharaoh na kutambua kazi yake sehemu ya profession waliandika Mfalme,na mwili huo ulipofika Ufaransa ulipewa heshima yenye hadhi ya kiongozi wa nchi kwa kuandaliwa gwaride maalumu la wanajeshi na heshima zote apewazo mkuu wa nchi.

Pharaoh anatajwa kuwa na watoto 200 na mwili wake ulipatikana mwaka 1881 kabuli lake lilikutwa na vitu vingi sana (kaburi lake lina zaidi ya ukubwa wa nyumba ya ghorofa yenye vyumba zaidi ya 6 ) ikiwemo maktaba ya vitabu 10,000 na perfumes nyingi.

 
ndio,mummies wengi wa Egypt inasemekana waliibwa sehemu za miili na hata dhahabu zao ziliibwa na wazungu
Wacha waibiwe tu sasa wanalala na mali wakati hawazifanyii kazi! Si Bora ikaletwa mtaani watu wanufaike nazo, hivi wenyewe hawana utaalum Kama wa wajerumani walivyofukia mali zao na kuweka mauzauza? Si wangeweka mauzauza kama wao kweli ustaarabu na maarifa yalianzia kwao basi elimu ya mauzauza wangekuwa nayo.
 

hiyo elimu wanayo mkuu[emoji16].kuna jamaa waliiba dhahabu kwenye hayo makaburi wakafa vifo vya ajabu
ila ulichosema ni kweli,kama Misri ya kale ingetunza yale ma dhahabu leo wangekuwa mbali sana
 
hiyo elimu wanayo mkuu[emoji16].kuna jamaa waliiba dhahabu kwenye hayo makaburi wakafa vifo vya ajabu
ila ulichosema ni kweli,kama Misri ya kale ingetunza yale ma dhahabu leo wangekuwa mbali sana
dhahabu mbona bado wanazo, na makaburi yapo, pyramids zipo, na egypt ndio nchi inayoongoza kwa kutembeleawa na watalii wanaoenda kuangalia pyramids
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…