Baada ya kutafisri Firefox kwa miezi minne, niliamua kujikumbusha PHP kidogo. Kwa hiyo mwisho wa wiki huu likaipeka tovuti ya tzLUG shopping na kupiga pasi baadhi ya kurasa.
Kurasa nilizifanyia kazi zaidi ni ya kuonyesha Linux Distrotulizonazo na matoleo yake. Pia nimebadili muonekano wa tovuti nzima. Nimekurahisisha uchaguaji wa Linux na toleo unalolitaka. Sasa unaweza kupata FreeBSD na openSolaris, ambazo sio Linux ila ni chanzo huria (open source). Ushindwe wewe tu.