Wakuu, humu JF nilikuwa napata story kuhusu sayari na nyota (solar system). Ilikuwa ngumu kuelewa kuwa jua letu ni mojawapo kati ya mamilion ya nyota (majua) na dunia yetu ni mojawapo ya mabilioni ya sayari (planets).
Kwa kuangalia picha hizi nimepata uelewa mkubwa sana tena kwa urahisi sana. Elimu haina mwisho aisee
Click hii link jielimishe huku ukifurahi, anzia picha picha ya kwanza hadi ya 26 kuelewa the story
Hapana hicho ni kile kimondo ambacho probe imetua mwezi huu, kipo baada ya Mars, ila kuna wakati kinakuwa baada ya dunia, orbit yake imekaa kiana. Link imewekwa sasa
Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa. (6)Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna. (7)Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea. (8) ##SURAT QAF
Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua. (47)Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi! (48)Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. (49)
##SURAT ADHARIYAT
Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga! (27)Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. (28)Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake. (29)Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. (30)
## SURAT ANAAZIAT