Pato la taifa la Uganda (GDP) yaizidi ya Tanzania kwa mwaka 2025 kwa mujibu wa shirika la fedha duniani -IMF

Daaah, mwaka 2025 ndio kwanza umeanza, wametupita lini sasa?!
 


Tanzania ni shamba la bibi lililopo karibu na shule .
Pato kubwa lipo mifukoni mwa watu wachache wenye kamba ndefu .

Kama kuna mahoteli ya kitalii huko Lokiondo na Liwale ambayo watalii wanalipa Mabilioni ya pesa kila siku lakini zinaishia mifukoni mwa wanaoitwa wawekezaji wakishirikiana na familia zisizozidi tatu ,huku wanyonge wakizidi kukamuliwa kwa kodi na tozo .Bila shaka kuna wakati mpaka Burundi itatipita kiuchumi.
 
Nyie Wanasiasa
 
Vipi upande wa kupima welfare na standard of living?
Kama nilivyotangulia kusema GDP haipimi maswala yanayohusiana na quality ikiwemo hivyo ulivyovitaja.

Formula ya GDP
Nominal GDP = C+I+G+(X-M)
C=consumption
I=investment
G=government expenditure
X=export
M=import

GDP PPP = Nominal GDP x (Market exchange rate/PPP exchange rate)

PPP exchange rate =
basket of goods price in one country/basket of goods price in another country

Kwa hizo formula GDP haiwezi tumika kuelezea mambo ya welfare, standard of living, income distribution, social equality nk.

Ila Tu inatia picha ya jumla ya uchumi WA nchi, na serikali nyingi hupenda kutazama progress ya uchumi Kwa kutazama nominal GDP. Hayo mengine kuna Kipimo ninaitwa GINI coefficient.
 
Nyie Wanasiasa
Sio wanasiasa .
Huo ndio ukweli ndio maana Magufuli alitaka tuwe na mfumo mmoja wa kukusanya mapato ya nchi na pia mama alipoingia alielekeza hivyo ila baadae akakaa kimya kwa sababu ya uchaguzi .

Kuna nchi zinaendesha bajeti zake kwa utalii.
Tanzania hata Takwimu ya watalii haiendani kabisa na hali halisi.

Kila kitu tukiwaachia wanasiasa matokeo yake wanakua mpaka juu ya uhai wa watu .
Siasa ni kazi kama kazi nyingine ni lazima tuwaseme na kuwakemea maana ndilo tabaka linalonufaika zaidi kwa kodi na pato la nchi
 
Kwani tuna mifumo mingapi ya kukusanya Kodi? Inahitaji miaka mingapi kuwa na huo mfumo ikiwa miaka 6 Bado ni kusema alitaka alitaka?

Mwisho haiwezekani hela zilipwe mifukoni Kwa watu wakati Kuna mamlaka ya kukusanya Kodi.

Kama wanakwepa ujue ni kama wewe unavyokwepa Kodi kwenye mambo Yako.
 
Kwani Kafulila anasemaje? Hakawii kusema hiyo taarifa ilikosewa😎😎
 
nyinyi si mumekubali kuimbishwa IYENA IYEEENA IYEEENA huko kwenu kila baada ya miaka 5., Nchi yoyote duniani kupitwa ni Uganda kiuchumi ni aibu na fedheha kubwa mno, Uganda imetengwa na kila mtu itapita vipi pato lenu la Taifa., muna bahari, madini na kila kitu
 
Nilifikir sisi ndo tutaiovertake Kenya kumbe sisi ndo tunaachwa na Uganda🤦🏾‍♂️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…