Patrick Aussems ameibadilisha sana Simba SC

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Mwanzoni Simba ilikuwa inacheza pasi fupifupi na taratibu baada ya ujio wa Patrick aussems Simba inacheza pasi za haraka na counter attack.

Lakini pia kitendo chake cha kuwapa nafasi karibia wachezaji wake wote kwenye kikosi chake kwa lugha nyingine anafanya rotation makocha wachache Sana wanafanya hiv. Ila kwenye CAF champion league ameangushwa na usajili wa miemuko wa viongozi wa Simba.

Hivi inaingia akili kwel unamsajili Deo Kanda mcheza na jukwaa unamuuacha Okwi mzee wa kazi,unamuuacha Haruna Niyonzima unamsajili Shubob wakati kulikuwa hakuna ulazima wakufanya hivo,wale wabrazili ndo takataka kabisa hata sitaki kuwazungumzia unaona kazi anayofanya Kenneth Juma anajua kutumia urefu wake vizuri anawin mipira yote ya juu tumeona kwenye mech ya Jana kiasi ambacho Wawa akawa kama yupo likizo lakini Lile librazili Gerson ni mrefu lakini hajui kutumia urefu wake lakini mara nyingi anakuwa out of position.

Unaenda kumsajili kiungo wa kibrazili ambaye hata robo ya uwezo wa Kotei hana hii ni akili au matope.

NB: next time uongozi wa Simba msifanye usajili wa miemuko ili mumsaidie Patrick Aussems kufanya kazi yake kwa ufanisi.
 
Mbona ausens alisema kuwa aliwahitaji okwi na kotei, lakini wachezaji wenyewe walitaka kutafuta changamoto nyengine kwengine, hivyo hawakuwa tayari kuongeza contracts zao. Na pia wachezaji wote walioachwa ni hao wawili tu kocha ndo aliyekuwa ana mipango nao, na ndo aliyowazungumzia.
 
Okwi na kotei kosa walilofanya viongozi ni kuacha mikataba yao iishe lakini viongozi waliwabembeleza mno mwisho wa siku wenyewe wakaamua kubadili upepo

Kuhusu niyinzima kocha alisema niyo na chama wanacheza mpira wa aina moja hivyi lazima mmoja kati yao aachwe ili apatikane kiungo mwenye uchezaji wa tofauti na hao wawili hata hivyo simba hawkutaka kumuacha walipokuja mezani haruna akataka dau kubwa ikabidi simba wamteme ukizingatia pia nidhamu yake haikuwa nzuri

Kwa mechi chache walizocheza wabrazil wawili naona wakiongeza kiwango kila uchao
 
Mimi kwa upande wangu naona Shiboub na Tairone wapo vizuri ila kwa Deo Kanda na Fragas pale Simba kala za uso. Na huyo Wilker bado hatujui uwezo wake maana kacheza chini ya dakika kumi tu tangu ligi ianze.
 
Kabla kuanza kulaumu muwe mnafatilia habari...kwa akili yako unafikiri Simba waipenda kuwaacha Okwi na Kotei.

Wachezaji wenyewe hawakutaka kuongeza mikataba walitaka kuondoka baada ya kupata ofa nzuri team nyingine..
Okwi alishasema akishindwa atarudi tena simba kama wakiwa bado wanamuhitaji.

Kati ya wale Wabrazil yule Beki mrefu mbona anacheza vizuri na ametulia huwa anawin dual ball zote..siku akicheza tulia muangalie anavyocheza.

Halafu Shiboub unamuangalia vizuri kweli anavyocheza? hebu tulia kijana angalia anavyocheza upate burdani.
 
Kweli ukiona tulitolewa ligi ya mabigwa africa sio kwamba tulikua hatuko vizur lahasha nazani ni makosa ya mtindo wa mpira kutoka kwa wachezaji wachache kam akina deo kanda hawakuwa wanachez kam kutaft magoli bali jukwaaa ziliwazid

1/ moja simba haikutegemea kam caf itatoa kwa ratiba kuanza kabla ya ligi kuu kuanza hilo lilikua tatizo kubwa ingawa tulijiandaa

2/ mtazamo wangu naona kiungo wa kibrazil anacheza mpira mzur anakaba hana madoido mengi uwanjan anagusa na kutoa anaenda kupeleka mashambuliz anarudi kukaba pia hicho ndio kitu cha kiungo mkabaji

3/ kuhus staiker wetu mbrazili kwa mtu anaejua mpira utajua jamaa anajua anadribo kali anacontorl nzuri ananguvu ngoja tusubir akipewa nafac zaid

4/ tunapat matokeo mazuri kwanini tuwalaum wachezaji tunatak kipi tena mbona wabongo hamukomi kila kukicha siasa za vijiweni mnatak kuujua mpira kam akina amunike kisa kucheza Barcelona akaona kila kitu anakijua

5/This is simba ushindi niwetu majungu tuache
 
Mimi bana hunitoi yanga. ila hapa umesema kweli mtani. Simba ilihitaj maboresho kidogo tu ili msimu huu waendelee walipoishia ila wamefumus kikos chote ndomana timu imeanza upya tena. Kama kikos kingebski vilevile na kuboreshs tu safu ya ulinzi basi mwaka huu ingekuwa semi final kama si final kabisa. Ila bado simba iko poa
 
Ulichoongea ni ushabiki wa kijinga tutaona hao wabrazili Kama watadumu hapo Simba zaidi ya mwaka mmoja
 
Mtoa post ni mkurupukaji sana! unataka nini zaidi ya timu inavyofanya sasa? kuhusu wachezaji wenu akina OKWI tusingeweza kuwa nao milele ni lazima ingefika wakati tungewaacha tu!! vijana waliopo sasahivi wote wazuri na ndo maana kocha ana uwezo wa kuwatumia yoyote kufuatana na uhitaji wa match kitu ambacho msimu uliopita kisngewezekana.
 
Kwa Fragas na Deo Kanda sijui wenzangu mnatumia vigezo gani. Wachezaji wapya wanaposajiliwa tunategemea wawazidi wale waliowakuta na waliondoka. Tukianza na Fragas je anakitu gani cha kumzidi sana Mkude pamoja na mapungufu yake? Je Kotei angekuwepo huyo Fragas angemuweka benchi. Tukija kwa Deo Kanda tulitegemea yeye ndio azibe pengo la Okwi lakini maajabu Miraji Athumani ndio anaziba pengo.

Tunapowazungumzia Deo Kanda na Fragas hatuna maana ni wachezaji wabaya hapana bali ni wachezaji ambao waliletwa ili kuiongezea Simba ufanisi lakini viwango vyao ni vya chini kulinganisha na wachezaji wazawa na wageni wenzao waliowakuta. Kwani tunategemea mchezaji mgeni akija alete ufundi ambao utawapa changamoto wachezaji wazawa. Na kwa Deo Kanda ndio kwanza benchi linamhusu atamfuata mwenzie Kahata kwenye mbao ndefu muda si mrefu kadiri injini ya Miraji inavyopata moto.

Ni wakati sasa viongozi wa Simba wakae chini na Miraji wamuongezee mshahara na marupurupu na wamfunge mkataba mpya wa muda mrefu wenye maslahi kwa pande zote mbili kwani umri unaruhusu na ameonyesha uwezo mkubwa kuliko hata wachezaji wa kigeni.

Na viongozi wasilaumiwe kwani unaweza kumuona mchezaji ni mzuri kwenye timu nyingine ukamsajili kwenye timu yako akacheza chini ya kiwango. Hata vilabu kama Barca, Madrid, Man U n.k. huwa vinakutana na tatizo hili.
 
Ulichoongea ni ushabiki wa kijinga tutaona hao wabrazili Kama watadumu hapo Simba zaidi ya mwaka mmoja
Kwa Fragas naona kama kweli hawezi kudumu. Ila yule beki Tairone yule bado yupo sana Simba kwa jinsi nilivyomuona uchezaji wake kwenye hizi mechi chache za kimashindano. Yule mshambuliaji Wilker ni mapema sana kusema chochote mpaka acheze walau mechi tatu za kimashindano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…