Paukwa!

Paukwa!

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Hadithi Hadithi!

Baada ya kuhitimu shule ya msingi nilifanya kazi za uvuvi kwa miaka mitatu.

Kisha nilisoma kozi za FETA za Refrigeration and Air conditioning. Nilianza na National Vocational Award (NVA) Level I (zamani Grade III) ya Refrigeration and Air conditioning. Baada ya miaka mitatu nilihitimu NVA Level III (Zamani Grade I).

feta-programs.png
Chanzo: FETA

Kwa mujibu wa Tanzania National Qualifications Framework (TzQF), elimu ya kiwango cha NVA Level III (Zamani Grade I) ni sawa na elimu ya kidato cha nne. Au tuseme kidato cha nne ni sawa na NVA III...

QualificationsFramework.png
Chanzo: Chapisho la Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, TCU.

Nikajiendeleza zaidi kwa kusoma miaka mingine miwili kozi ya Fish Processing and Marketing katika ngazi ya National Technical Award (NTA) Level 4 na 5. Kwa mujibu wa Tanzania National Qualifications Framework (TzQF), elimu ya kiwango cha NTA Level 4 na 5 ni ZAIDI ya elimu ya kidato cha nne, na ni sawa na elimu ya kidato cha sita.

Baada ya hapo niliajiriwa kwenye makampuni binafsi ya kuchakata minofu ya samaki, na kupata uzoefu wa miaka miwili.

Kutokana na uzoefu nilioupata kwenye kazi, nilijiendeleza zaidi katika ngazi ya Diploma, yaani, NTA Level 6, katika nyanja za Fisheries Resource Management and Technology. Kwa mujibu wa Tanzania National Qualifications Framework (TzQF), elimu ya kiwango cha NTA Level 6 ni ZAIDI ya elimu ya kidato cha sita. Baada ya kuhitimu diploma, nimefanyia kazi maarifa niliyopata kwa miaka mitatu sekta binafsi ya uvuvi.

Hivi karibuni niliona tangazo la Tume ya Ajira kuhusu nafasi ya Research Technician II. Ninao uzoefu na sifa zote kwa ajili ya kufanya kazi hii. Lakini ninashindwa kuomba kazi hiyo kwa vile sina cheti cha kidato cha nne au cha sita, hata kama TzQF inaniona ninayo elimu kubwa kuliko kidato cha nne au cha sita. Fursa zilizopo ni kwamba, nikasome QT na kusiti mtihani wa kidato cha nne, nipate angalau "D" mbili za Kiswahili na Bible Knowledge, na kutumia miaka mingine miwili. Au kwamba Utumishi wa Umma nitaendelea kuusikia tu kwa vile nilisoma elimu 'ya kambo' ambayo haikupitia vidato vya sekondari. Au niende nikasome shahada ya kwanza vyuo vya hapahapa? Pana chuo kingine kimenipa fursa ya kusoma shahada ya uzamili (Masters) kwa kuangalia vyeti nilivyonavyo na uzoefu. Lakini kiko nje ya nchi. Lakini vyote hivyo havitafaa kitu kwa vile sina cheti cha kidato cha nne.

Mwisho wa HADITHI.

REJEA:

Elimu ya Ufundi Katika Utumishi wa Umma

Watumishi wasio na vyeti vya ufaulu kidato cha nne lakini...


 
Back
Top Bottom