Paul Clement ashauriwe, Asaidiwe, aombewe!

Paul Clement ashauriwe, Asaidiwe, aombewe!

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Nikiri wazi mimi ni mmoja wa watu wanaompenda na kumfuatilia kwa karibu sana muimbaji wa Injili Paul Clement,
Toka enzi zile akiwa na glorious mpaka sasa akiwa solo artist..

Kwa hakika kijana huyu ana kipaji cha hali ya juu mno.
Lakini kwa miaka ya hivi karibuni toka aanze kuimba live amekuwa akizidisha mno kuyumbisha sauti yake kwa "minor" zisizokuwa na ulazima wowote na kupelekea kuharibu nyimbo zake yeye mwenyewe.

Ni wakati sahihi wa waimbaji wakongwe kukaa na kijana huyu na pasipo kumuonea aibu wamchane Ili arudi katika sauti yake halisi.
Anazidisha mbwembwe mnoo.
Kwa walioangalia au kuhudhuria Christmas carols ya tar 19 pale milimani city basi wataungana na mimi kuwa mmojawapo ya show mbaya Zaidi ilikua ni ya Paul,
Binafsi nakuombea urudi tena katika uimbaji wako kama Identity Yako acha kuiga iga wahuni.

Nakuombea.
 
Mziki wa injili ni biashara, na kwa sasa soko linataka uimbaji wa aina ile.
 
Sisi tuliokuwepo hatujaona tatizo shida moja ya paul hajui kuichangamsha hadhira yaani hana vibes nimehudhulia concert ambazo amehudumu kama 3 hiyo ndo shida yake kubwa niliyoiona
 
nyie watoto wa clement mnataka kutuingiza cha kike??, wewe allan si useme tuu unatafuta msaada wa mdogo wako paulo??
 
Nikiri wazi mimi ni mmoja wa watu wanaompenda na kumfuatilia kwa karibu sana muimbaji wa Injili Paul Clement,
Toka enzi zile akiwa na glorious mpaka sasa akiwa solo artist..

Kwa hakika kijana huyu ana kipaji cha hali ya juu mno..
Lakini kwa miaka ya hivi karibuni toka aanze kuimba live amekuwa akizidisha mno kuyumbisha sauti yake kwa "minor" zisizokuwa na ulazima wowote na kupelekea kuharibu nyimbo zake yeye mwenyewe..

Ni wakati sahihi wa waimbaji wakongwe kukaa na kijana huyu na pasipo kumuonea aibu wamchane Ili arudi katika sauti yake halisi..
Anazidisha mbwembwe mnoo..
Kwa walioangalia au kuhudhuria Christmas carols ya tar 19 pale milimani city basi wataungana na mimi kuwa mmojawapo ya show mbaya Zaidi ilikua ni ya Paul,
Binafsi nakuombea urudi tena katika uimbaji wako kama Identity Yako acha kuiga iga wahuni...
Nakuombea.
Mbona yuko vizuri tu, U Mwema umeisikia? Ngoma kali, full upako...na ile chombo kaimba nayo sijui kaitoa wapi
 
Wewe ni mwema, u mwema......nabarikiwa Sana na huu wimbo wake hebu niusikize huenda nikapona hii omicron
 
Sisi tuliokuwepo hatujaona tatizo shida moja ya paul hajui kuichangamsha hadhira yaani hana vibes nimehudhulia concert ambazo amehudumu kama 3 hiyo ndo shida yake kubwa niliyoiona
Hivi kwenye nyimbo za kuabudu pia Kuna kuchangamsha..
 
Sisi tuliokuwepo hatujaona tatizo shida moja ya paul hajui kuichangamsha hadhira yaani hana vibes nimehudhulia concert ambazo amehudumu kama 3 hiyo ndo shida yake kubwa niliyoiona
Akuchangamshe tena jamani ? Ungesema akiimba hauhisi uwepo ningekuelewa. Huduma yake imebase kwenye ku-worship zaidi ni kuita uwepo wa Mungu Sasa kazi Ni kwako Kuji-connect .
 
Back
Top Bottom