Wajumbe,
Hili dude la mkataba wa DP World na Serikali ya Tanzania ina makando-kando mengi. Katika kufukunyua nimekutana na wavaa miwani mieusi tena ni PSU.
Huyu Bwana amenidokeza kwamba katika uwekezaji huu Rwanda ya Paul Kagame anayo hisa 17% katika kampuni ya DP World na ndiye amekuwa na ushawishi mkubwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika ziara ya Kagame siku za karibuni ilikuwa ni kukamilisha dili lenyewe. Ikumbukwe Kagame amekuwa na hamu ya kumiliki Bandari ya Dar es salaam kwa miaka mingi akiamini kwamba "tumeshindwa kutumia Bandari ya Dar es salaam kutuletea faida".
Hata hivyo, mtoa habari huyo amedai hatua hiyo haijamfurahisha Jakaya Kikwete na ndiye yuko nyuma ya wapinzani wa mkataba huu wa kifedhuli.
Paul Kagame, Rais wa Rwanda
Sultan Ahmed Bin Sulayem, Kiongozi Mkuu wa DP World
Hili dude la mkataba wa DP World na Serikali ya Tanzania ina makando-kando mengi. Katika kufukunyua nimekutana na wavaa miwani mieusi tena ni PSU.
Huyu Bwana amenidokeza kwamba katika uwekezaji huu Rwanda ya Paul Kagame anayo hisa 17% katika kampuni ya DP World na ndiye amekuwa na ushawishi mkubwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika ziara ya Kagame siku za karibuni ilikuwa ni kukamilisha dili lenyewe. Ikumbukwe Kagame amekuwa na hamu ya kumiliki Bandari ya Dar es salaam kwa miaka mingi akiamini kwamba "tumeshindwa kutumia Bandari ya Dar es salaam kutuletea faida".
Hata hivyo, mtoa habari huyo amedai hatua hiyo haijamfurahisha Jakaya Kikwete na ndiye yuko nyuma ya wapinzani wa mkataba huu wa kifedhuli.
Paul Kagame, Rais wa Rwanda
Sultan Ahmed Bin Sulayem, Kiongozi Mkuu wa DP World
- Tunachokijua
- Tangu taarifa za Tanzania kuingia mkataba na Kampuni ya Dubai ya DP World kuanza kuenea mnamo Juni 5, 2023 mwaka huu na Azimio la mkataba huo lilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Junii 10, 2023, kumekuwa na hoja nyingi zimeibuliwa miongoni mwa Wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Sehemu za hoja hizo zimejigawa katika makundi mawili ikiwamo wanaopinga kusainiwa kwa mkataba huo wakidai una mapungufu mengi na upande mwingine wanaunga mkono wakiona kwamba mkataba huo una maslahi kwa taifa.
Zaidi ya kuwapo hoja za kupinga na kuunga mkono mkataba huo, pia kumekuwepo na hoja nyinginezo ambazo Wadau mbalimbali wamekuwa wakizitoa ikiwa kama ni sehemu ya kuwafanya wengine waelewe mambo mengi zaidi. Mfano, mnamo Julai 14, 2023 Mwanachama wa JamiiForums Desprospero amekuja na hoja akimuhusisha Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuwa Mwanahisa wa Kampuni ya DP World. Sehemu ya andiko hilo Desprospero ameeleza:
Paul Kagame anayo hisa 17% katika kampuni ya DP World na ndiye amekuwa na ushawishi mkubwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Katika ziara ya Kagame siku za karibuni ilikuwa ni kukamilisha dili lenyewe. Ikumbukwe Kagame amekuwa na hamu ya kumiliki Bandari ya Dar es salaam
Je, Madai ya Paul Kageme kuwa na hisa DP World yametokana na nini?
Uvumi huu umezaliwa kutokana na kauli ya Rais Kageme 2014 ambayo ilionesha matamanio yake kuwa na Bandari kama Dar es Salaam. Kagame alieleza kuwa kama Rwanda ingekuwa na bandari kama Dar es Salaam basi huduma zote nchini Rwanda zingekuwa bure. Baadhi ya wadau wanaichukulia kauli hii kama ni mwanzo wa Kagame kuitaka bandari ya Dar es Salaam.
Pia madai haya yalikolea zaidi baada ya kubainika kuwa mnamo tarehe Desemba 17, 2020 DP World ilisaini makubaliano ya kuendesha bandari Kavu nchini Rwanda. Wadau wanaomuhusisha Kagame na DP World wanaona kama makubaliano haya yalikuwa ni kama kutengeneza mazingira na maandalizi ya DP World kumiliki bandari ya Dar es Salaam.
Zaidi ya hayo, madai ya Paul Kagame kuhusishwa na DP World na Bandari ya Tanzania yanachochewa na ziara ya Rais Paul Kagame nchini Tanzania mnamo Aprili 27, 2023. Wadau wanaihusisha ziara hii na Rais Kagame kuja kuwaandalia mazingira DP World.
Hata, hivyo JamiiForums baada ya kupitia madai na hoja zote za wadau hawa, tumebaini kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoweza kuthibitisha hoja zao.
Je Paul Kagame nyuma ya DP world?
Baada ya kuletwa kwa hoja hii JamiiForums imepitia katika vyanzo na taarifa mbalimbali ili kupata ukweli kuhusu Kagame kuhusika na hisa ndani ya kampuni ya DP World kama ifuatavyo:
Katika ukurasa rasmi wa DP World wameweka taarifa zote za msingi ikiwamo miradi yao na orodha ya viongozi wa kampuni wao huku Sultan Ahmed Bin Sulayem, akitambulika kama kiongozi mkuu wa kampuni hiyo. Sehemu hiyo pia inaorodhesha Viongozi wote wa Bodi wa kampuni hiyo lakini haisemi chochote kuhusu umiliki wa hisa wala haimuoneshi wala kumtaja Paul Kagame sehemu yoyote.
Pia Taarifa ya Jarida la The Guardian zilizochapishwa mwezi Machi, 2022 zinaeleza kuwa Kampuni hiyo inamilikiwa na Familia ya kifalme ya Dubai huku pia ikimtambua Sultan Ahmed Bin Sulayem kama kiongozi wa juu wa familia na mmiliki wa kampuni hiyo. Licha ya Jarida hili kueleza kwa kina juu ya historiana Wamiliki wa Kampuni ya DP World, hakuna sehemu yoyote andiko hili limedokeza chochote kuhusu Kagame kumiliki au kuwa na hisa kwenye kampuni hiyo.
Nao, ukurasa wa habari za biashara wa Market Screener hautofautiani na vyanzo viwili hapo juu. Ukurasa huu umeeleza kwa kina kuhusu Viongozi wote wa Kampuni ya DP World ikiwamo na watu wote walio katika Bodi ya Kampuni hiyo. Hata hivyo katika taarifa zote hakuna sehemu ambayo inaonesha Paul Kagame wa Rwanda kuwa sehemu ya wamiliki au Wanahisa wa kampuni hiyo.
Hivyo, kutokana na kupitia vyanzo hivyo rasmi na kuaminika JamiiForums inaona kuwa uvumi unaomhusisha Paul Kagame kuwa muhusika na mwanahisa wa Kampuni ya DP World ni uzushi.