Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 855
Economies of scale cannot get any better!
He deserves it.
Also, he deserves a Pulitzer for his NYTimes columns.
And a gold star for putting Bush's admin in its place.
``Mr. Bush has degraded our government and undermined the rule of law,''
Who else could have put it more congruous?
GT, lakini huyu na wenzake wengi waekonomia si ndiyo waliotuweka kwenye hii crisis hivi sasa?! Chumi nyingi duniani zimefata mfumo wa Marekani na sasa hivi tumeona makosa mengi tu ambayo yangeweza kabisa kuepukika... si ni ndiyo hawa hawa wa kulaumu au?!
And whats fav Krugman book?
GT, lakini huyu na wenzake wengi waekonomia si ndiyo waliotuweka kwenye hii crisis hivi sasa?! Chumi nyingi duniani zimefata mfumo wa Marekani na sasa hivi tumeona makosa mengi tu ambayo yangeweza kabisa kuepukika... si ni ndiyo hawa hawa wa kulaumu au?!
Have there ever been African Nobel Laureates in scientific endeavors such as economics, physics, chemistry, medicine, etc? If not why not? Can someone come up with plausible reasons?
Have there ever been African Nobel Laureates in scientific endeavors such as economics, physics, chemistry, medicine, etc? If not why not? Can someone come up with plausible reasons?
SteveD,
Hapana, huyu mzee theories zake zinafanya kazi. Moja ya theories zake muhimu ni ile ya economies of scale. Inafanya kazi kazi kila sehemu bila kujali ni kwenye ubepari au ujamaa. Wachina sasa wanaitumia mno na kuijaza dunia kwa vitu vyao kwa bei ya chini kabisa. Tatizo tu ni kushuka kwa quality.
Waliotuingiza kwenye haya matatizo ni wale watumiaji wa theories za wachumi ambao baada ya kuona zinafanya kazi wakaanza kuzitumia na kuzidisha ulafi.
Waafrika wengi hawajapata nishani za Nobel sababu wasomi wengi wa Afrika wengi ni historians.Wanangoja wengine wagundue kitu waandike halafu wao wachukue hivyo vilivyoandikwa na kuanza kuvielezea kwa mbwembwe za msomi bwege.Kila msomi wa kiafrika akitaka kuelezea kitu lazima ataje refference ya kitabu kilichoandikwa na mzungu fulani wa Ulaya au marekani kama siyo ubwege ni nini.Mtu huwezi kichwa chako mwenyewe kikawa refference hadi ufanye refference kichwa cha Mzungu ?
Mfano injinia ,daktari,mchumi,n.k wa kiafrika anachofanya ni kusoma vitabu vilivyopitwa na wakati vya hizo fani walivyoandika wagunduzi wa Ulaya na Marekani na kuvikariri barabara ili afanye vile vitabu alivyosoma vilivyosema.Atang`ang`ania hivyo hadi litoke toleo lingine (NEW EDITION) ya huko kwa wazungu walikogundua! Ndipo naye abadilike na kubadili msimamo na kujifanya msomi wa kisasa mwenye wazo jipya!
Wenzetu Ulaya na Marekani huwa wagunduzi sababu huwa hawaogopi kwenda nje ya maktaba ya vile vitabu walivyosoma vinavyosema .Huwezi kuwa ni mtu mwenye mawazo mapya kama kazi yako ni kukariri tu kazi za vitabu vya wengine .Tunahitaji watu wawezao kuwaza nje ya vitabu pia wakaja na ugunduzi mpya na wao wakawa.
Kazi ya vitabu na shule na vyuo ni kuamsha uwezo wa mawazo mapya.Afrika ni bahati mbaya kuwa msomi hana kazi ya kuwaza mawazo mapya zaidi ya kuelezea mawazo ya vile alivyosoma vya wengine!
Waafrika wana uwezo mkubwa mno wa kukariri iwe biblia,kurani,au vitabu vya fani za sayansi n.k lakini ni wavivu mno wa kufikiri mawazo mapya au kugundua vitu vipya.Ikija kufikiri vitu vipya si ajabu kukuta hata msomi profesa anakuwa ni sifuri.
Mtaalamu mmoja wa filosofia aliwahi kusema kuwa pamoja na elimu rasmi kuwa ni nzuri lakini imeua uwezo wa ugunduzi wa mambo mapya ya mamilioni ya wanadamu waliosoma elimu rasmi hasa katika bara la Afrika.
Kila msomi wa kiafrika akitaka kuelezea kitu lazima ataje refference ya kitabu kilichoandikwa na mzungu fulani wa Ulaya au marekani kama siyo ubwege ni nini.Mtu huwezi kichwa chako mwenyewe kikawa refference hadi ufanye refference kichwa cha Mzungu ?
Ninaamini kuwa kureference paper au kitabu kilichoandikwa na mtu mwingine is crucial in backing up one's findings and has nothing whatsoever,to do with one's failure to be creative.Kwa mfano,kama unaclaim kugundua theory mpya on how one's nick name reflects his ability to analyze opinions different from his stand point,ni vizuri ukaonyesha proof kwamba hakuna mtu mwingine ambaye ameshaelezea theory kama hiyo.In reality,wanakuwepo na ideas zao zinaweza kutofautiana na za kwako kwa kiasi fulani,you need to show the difference by making a comparisons between the two.Katika kufanya hivyo ni lazima ufanye referencing ya kazi ya huyo mwandishi mwingine.
Waafrika kureference kazi za watu wa magharibi,not acceptable to you,I get it.Vipi kuhusu waafrika kureference kazi za waafrika wenzao?What difference does it make as far as being ''creative'' is concerned?
Ninaolongelea mimi ni wale wabunifu wa vitu vipya na mambo mapya ambao hawahitaji reference kwenye kichwa chochote cha mtu mwingine awe mzungu au mwafrika wanapobuni vitu vyao vipya.Waafrika kwenye eneo hili ndio tuko nyuma sana ukilinganisha na Ulaya na Marekani.Hata wachina na wahindi sasa wameanza kutuacha mbali katika ugunduzi baada ya wao kugundua makosa yao na kuanza kuvitumia vichwa vyao barabara katika ugunduzi badala ya kukesha maktaba kufanya reference za watu wengine kama wasomi wa kitanzania walivyojijengea mazingira ya kubobea kwenye reference wakiwa hawana lao jipya la ugunduzi mpya.