Paul Mashauri, Amewaelezea vizuri Marehemu Mengi, Mufuruki, Chande, Musiba na Ruge

Nashukuru kwa muda wako nimejifunza mengi sana.

Nimependa changamoto za biashara alizotaja Abraham Mengi: Roho mbaya, Chuki na Wivu! Watu wanaona mbali kwa kweli
kitanzania Tanzania, ukiyaweza hayo matatu, mengine ni marahisi sana.
 
Huyu jamaa inaonekana anafahamiana na kila mtu. Sitashangaa siku Obama akifariki akatuelezea ya kufahamiana hadi na kina Kennedy.
 
Pia umesahau kwamba Andy Chande alikuwa kiongozi wa ngazi wa juu wa chama cha Freemasons hapa Afrika mashariki na ndio ukawa mwanzo wa urafiki na familia ya Malkia wa Uingereza ambaye mume wake Prince Philip ni kiongozi wa Freemasons,miaka ya nyuma kujitanabaisha kuwa wewe ni Freemasons ilikuwa sio jambo la siri,walikuwawanatoa hadi misaada mashuleni na kwenye hafla mbalimbali,kuna viongozi wengi na wafanyabiashara wakubwa ni wanachama wa Freemasons ingawa kwa sasa wengi wao wametangulia mbele ya haki na wengine ni wazee,jengo lao lipo pale nyuma ya Bima Kitega Uchumi na linatazamana na hoteli ya Kilimanjaro kwa nyuma.Ni hayo tu mkuu
 
Paul Mashauri umejitahidi ku- narrate hii kitu ila kuna exaggeration umefanya .

Hao wote walikuwa mabingwa Ila walikuwa na dark side zao. Kuna wengi waliumizwa sana na hao watu ili wao kufikia mafanikio hayo!

Wewe nakujua sana toka uko Chuo Kikuu pale Mlimani miaka ya 2002 - 2005 ulikoanza kupenda kuwa karibu sana na watu wenye mafanikio na publicity.

Nilikuona ulivyoanzisha lile gazeti lenu la Familia pale Millennium Business Park ukiwa huna focus nzuri na ku- create losses kwa Godfather wako na hili huwezi kulisema popote!

Najua wewe ni "inspirational speaker" siyo "motivational speaker" mzuri lakini unapenda ku- link sana tu - story ili kupata self attention!

Hivi wewe na Sir Andy Chande, wapi na wapi?!

Kama Jina la Elvis Musiba tu umelikosea na unasema kuwa ulikuwa naye karibu sana nani ataamini kuwa hii story yako si fabricated?! Jina lake la kati la " Tables" wewe ndo leo umenijulisha!

Kuhusu malipo ya Azim Jamal ni total exaggeration ! ! Million 10 usd per talk ni sawa na Tshs.23 billion, too much Bw.Speaker! Na eti wewe ni CEO wa makampuni,kitu kidogo kama hicho unashindwaje ku- notice!? Hata maguru kama Robin Sharma na the late Dr.Myles Munroe wangeshagaa malipo hayo kwa Motivational Speaker kwa event moja!

Anayepata hiyo income per event ni Floyd Mayweather ( mpiga ngumi wa Marekani) na ma super star wa kariba yake!

With my experience watu lazima wawe makini sana na " Inspirational speakers" wa Bongo ,the Paul Mashauri type kwani mnaweza kuwa mis- lead watu na empty stories zenu !

Hawa unaweza kuta amefanya make- up na mke wake na waka- cover front page ya magazine fulani kama best couple in town and the next day ukaambiwa wametengana (divorce) kama mume na mke!

Many! many !many! Untold dark stories!
 
dark side ndio zilizowapa mafanikio na huwa hawazisemi
.. mambo wanayoyasema wengi tunayajua tayari
 


Ukisikia alichosema Paul kutoka kwa Mengi, ukiweza kushinda roho mbaya, chuki, na wivu ndo huu sasa!

Watu mnawazaga negative tu siku zote. Mfano aliposema Jamal analipwa 10 ml US$ sawa na 20ml Tsh kwa nn usione hayo ni makosa tu ya kihesabu kwamba kashindwa kufanya exchange rate ya Tsh 20 mil ni Dollar ngapi?

Kwa hela halali aliyoandika hapo ni Tsh 20,000,000 ambayo na uhakika alitaka kusema analipwa 10,000 US$ per talk.

Tukiweza kuwa positive na "kushinda Wivu, Roho mbaya, na Chuki tutaweza kufikia malengo ya maisha yetu" Mr Mengi.
 
Aisee
hivi ndugu,
Ni wangapi waliosoma Ila bado ufunguo wa maisha hawajaupata,hebu tuwe positive katika kuangalia mambo,yeyote atakaecopy na kupest haya maneno ya motivation speakers lazima ile kwake,ila kwa yeyote anae yaangalia akayapima vizuri pale kwenye walakini akaingia in deep kupata taarifa sahihi ni tofauti na ambae hata hizi kauli za motivspeaker hakuzipata,mifano ipo watu walisoma/kuwasikiliza hawa jamaa wakatia juhudi binafsi wameweza kusogea.
Ni kweli hakuna asie na dark side,ila je hiyo darkside itakujenga?
Kuna mengi yanaweza kujaziwa humu kutoka kwenye haya machache yaliyoelezwa na huyu inspiration speaker na tukapata kitu,so please hebu nawe tuongezee kwa ufupi Yale machache unayofahamu +kuhusu hawa jamaa au wengine wanaoweza kuvuta akili za wanaopenda kujifunza.
Sikosoi mtazamo wako Ila najaribu kuupush uwe wenyenyama zaidi,mfano inawezekana unaelewa namna walivyotumia darkside zao vizuri kupenya kwenye tundu la sindano,au ubora wa elimu zao,vipaji n.k
Katika ulimwengu wa mafanikio kila taarifa uipatayo ni fursa inategemea umeipokea Vipi na kuielewaje.
 
Mambo mengi mema nimejifunza kwenye huu uzi. Sijali wala sitojali kujua kama yametungwa ama ni halisi. Cha muhimu nimeridhika na content.

Nyie mlioamua kuwa negative na huu uzi ati kwa kuwa hamumkubali Mashauri ni vyema mkatuacha tule chakula ya nafsi hapa.
 
Paul Mashauri... mabrazamen wa Forodhani Sec School mjini POSTA kitambo na hicho.... Huyu ni fundi wa maneno na kuweka watu kati.
 
...Ni Elvis Eristablus Musiba..,
 
Pamoja na kuwaelezea vizuri hao marehemu lakini siyo Elvis Tables Musiba ila ni Elvis Aristablus Musiba.
Ni kweli, jina lake ni Aristablus Elvis Musiba. Hiyo Tables sijui ameitoa wapi! Nimesoma vitabu vyake karibu vyote, kuanzia Kufa na Kupona to Kikosi cha Kisasi, sikuwahi kuona hilo jina la Tables!
 
Mwamba big up saanzzz nimekeshea uzi wako nitaufanyi kazi...

Roho mbaya chuki na wivu... mbele kwa mbele.... balls ni muhimu sana from Ruge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…