Paula Kajala: Mama hawezi rudiana na Harmonize, kasema bora afe akiwa single

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Paula Kajala amethibitisha rasmi kuwa mama yake, Kajala Masanja, amefunga kikamilifu ukurasa wa mahusiano na msanii wa muziki wa Bongo Flava, Rajab Abdul Kahali maarufu kama Harmonize, na kwamba hakuna uwezekano wowote wa wawili hao kurudiana tena.

Akiyafichua hayo kupitia mazungumzo na mfanyakazi na mtangazaji wa Wasafi, Juma Lokole, Paula alieleza kuwa hakuwahi kufurahishwa na vitendo vya mama yake kurudiana na msanii huyu hapo awali, lakini alilazimika kukaa kimya ili kuheshimu hisia na maamuzi ya mama yake.

"Kama kuna watu wamesubiri kuona mama amerudiana tena na Rajabu, basi niwaambie tu huo ukurasa tena haupo. Kwanza mimi sikuwahi kufurahishwa na mama kurudiana rudiana na Rajabu, ilikuwa ni basi tu kwa sababu niliheshimu hisia na maamuzi yake ila nilikuwa sipendi," alisema Paula.

Paula aliongeza kuwa mama yake amechukua msimamo mkali na kufanya uamuzi wa mwisho wa kutojihusisha tena kimapenzi na msanii huyo.

"Mama kashafunga huo ukurasa, kasema haitokuja kutokea arudiane na Harmonize, ni bora afe akiwa single. Na kitu kizuri zaidi nakuja na interview ya mama akieleza matukio yote toka alivyoanza mahusiano na Harmonize, watu wakae mkao wa kula," alisisitiza.

Ili kuweka kila kitu wazi kwa umma, Paula amewataka mashabiki na jamii kujiandaa kwa ajili ya mahojiano maalum ya mama yake yatakayoruka hivi karibuni, ambapo ataeleza kwa undani matukio yote yaliyojiri tangu walipoanza mahusiano yao hadi kufikia hatua ya kutengana kabisa.
 
Alimrudisha ili amfire kulipa kisasi?
 
Laana.

Mtoto haupaswi kuingilia mambo ya mahusiano ya wazazi wako!

Your browser is not able to display this video.
 
ALipoanza kuzungumzia kwamba kuna interview tukae mkao wa KULA ,nikakosa Power.

Kajala kwa Tembo hatoboi ,ngoja hiyo interview iishe uwaone tena wakijivinjari.
Kwa Tembo Huwa anafuataga Nini au ndo kashuka kiwango tayari?
 
Kwa hiyo mambo ya mahusiano yao ni chakula kwa umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…