Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul amesema kiwango cha adhabu kilichopendekezwa kwenye Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa Mwaka 2024, kwa wafanyabiashara watakaoshindwa kuweka wazi bei za bidhaa wanazouza, kiendane na ukubwa wa biashara husika.
Muswada huo umependekeza kuweka sharti la kila mfanyabiashara nchini kuweka hadharani bei ya kila bidhaa anayouza, na kupendekeza adhabu ya faini kati ya shilingi 10,000 hadi shilingi 1,000,000 kwa atakayeshindwa kufanya hivyo.
Akichangia muswada huo bungeni leo, Gekul amesema licha ya kushushwa kwa adhabu hiyo, bado inapaswa kuzingatia ukubwa wa biashara husika.