Paulo wa Tarso aliebuni Ukristo Baada ya Yesu

Tofauti ya yesu na paulo ni miaka 200 walikutana wapi, paul anasema amekutana na yesu kama anavyodai yule mfalme wa mwanza
kwenye mikeka ya ubwabwa na mnapocheza bao huwa mnadanganyana kwamba tofauti ya Yesu na paulo ni miaka 200. mmepungukiwa elimu na ufahamu hadi huwa hamjui mnachoongea.

kwa kukusaidia, wakati Yesu anahubiri Yerusalemu na kwengine, paulo pia alikuwa Yerusalemu chini ya kuhani na mwalimu Gamalieli aliyemfundisha dini na sheria za kiyahudi. pamoja na kwamba paulo alikuwa myahudi aliyezaliwa tarso ila aliletwa yerusalemu ili afundishwe dini, wakati yesu anakua na kuhubiri paulo alikua yerusalemu pia.

kuna mwanafunzi mmoja aliitwa stafano, huyu hakuwa mtume (among those 12) ila alikuwa mwanafunzi wakati yesu anahubiri miaka ile 3. Yesu alipopaa mbinguni, moja wa wanafunzi waliokuwa wakihubiri ukristo ni stephano. wayahudi waliamua kumpiga kwa mawe hadi akafa, na PAULO kama myahudi mwenye siasa kali alisimamia mauaji ya huyo stefano. baada ya mauaji ya stefano ndipo mitume na wanafunzi walikimbia na kusambaa maeneo mbalimbali, wengine walienda 'antiokia uturuki na hapo ndipo waliitwa kwa mara ya kwanza wakristo, yaani wafuasi wa kristo. so, paulo aliexist hata wakati stefano mwanafunzi wa Yesu alipouawa na yeye alikuwa kiongozi wa wauaji hao.

mara baada ya Yesu kupaa, wafuasi wake waliokuwa wakihubiri injili, wengi walinyanyaswa na kuuawa, paulo alikuwa kiongozi wa wayahudi wenye siasa kali waliokuwa wakiua wafuasi wa Yesu, meaning, paulo alikuwepo wakati Yesu anafanya huduma miaka 3 na alikuwa na umri sawa na ule wa wanafunzi wake au pengine alikuwa na umri mkubwa kuliko wao, na kama ni hivo basi paulo alikuwa na umri mkubwa kuliko Yesu kwa sababu Yesu alikufa akiwa na miaka 33, na wanafunzi wake wengi walikuwa na umri mkubwa kuliko yeye. hivo kusema paulo alikuja kuishi miaka 200 baada ya Yesu ni uongo wa baba yenu mwongo mood na babu yenu shetwan.
 
Shida ya ndugu yetu huyu mleta mada anaokoteza okoteza maandiko kujustify mawazo yake.
 

Sikiliza kwa makini, maana haya siyo maneno ya wanadamu bali ni neno la Mungu linaloleta uzima. Kwanza kabisa, hata tarehe unazotumia sasa zinashuhudia Kristo. Leo hii unaposema mwaka 2025, unakiri pasipo kujua kwamba dunia nzima inahesabu miaka kwa jina la Yesu Kristo kabla ya Kristo (BC) na baada ya Kristo (AD). Hii ni alama ya wazi kwamba Yesu si mwanadamu wa kawaida, bali ni Mwana wa Mungu aliyeweka historia yote chini ya jina lake. Hakuna Nabii, hakuna mfalme, hakuna mwanadamu yeyote ambaye historia yote imepimwa juu ya jina lake isipokuwa Yesu Kristo pekee.

Sasa unasema Paulo ndiye aliyebuni Ukristo huo ni uongo unaotoka kwa adui wa roho zetu. Yesu mwenyewe kabla ya Paulo hajawahi kuandika barua yoyote, alisema kwa uthabiti: “Nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda.” (Mathayo 16:18). Kanisa ni kazi ya Kristo mwenyewe! Paulo hakuwa muanzilishi, bali alichaguliwa na Bwana kama chombo cha kubeba injili kwa Mataifa. Ni Kristo aliyemfunulia, na mitume waliokuwa Yerusalemu walimkubali na kumpa mkono wa ushirika. Hivyo siyo Paulo aliyebuni, bali ni Yesu aliye hai aliyefanya kazi kupitia Paulo.

Kisha unasema Yesu hakufundisha juu ya kifo chake kwa ajili ya dhambi. Hilo pia ni upotoshaji. Yesu mwenyewe alisema: “Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia kwa wengi.” (Mathayo 20:28). Tena usiku wa kukamatwa kwake akasema: “Hii ndiyo damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.” (Mathayo 26:28). Maneno haya yalitoka kwa kinywa cha Bwana mwenyewe, kabla hata Paulo hajaanza huduma. Kwa hiyo kifo chake si jambo la kisiasa, ni mpango wa Mungu wa wokovu.

Ni kweli Wayahudi walipeleka mashtaka ya kisiasa mbele ya Pilato kwa sababu hawakuwa na mamlaka ya kisheria kumsulubisha mtu. Lakini kiini cha chuki yao hakikuwa kodi ya Kaisari, bali dai la Yesu la uungu. Soma Yohana 10:33, walimwambia waziwazi: “Si kwa tendo jema tunakupiga mawe, bali kwa kukufuru; kwa kuwa wewe u mwanadamu, wajifanya Mungu.” Hii ndiyo sababu kuu iliyowasha moto wa chuki, na kupelekea kusulubiwa. Hivyo hoja kwamba hakusulubiwa kwa madai ya uungu ni ya uongo kabisa, kwa sababu maandiko yameandika wazi.

Yesu alikuja kama mwanadamu ili apate kuchukua nafasi yetu. Ndiyo maana aliweza kusema “Mimi mwanadamu” (Yohana 8:40). Lakini huyo mwanadamu ndiye Neno aliyekuwepo tangu mwanzo, na Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu (Yohana 1:1). Neno hilo lilifanyika mwili (Yohana 1:14). Hii ndiyo siri ya umwilisho Mungu akawa mwanadamu kwa ajili ya wokovu wetu. Hii ndiyo injili yenye nguvu, injili isiyopingika, injili iliyojaa upako wa Roho Mtakatifu.

Kwa hiyo sema nini useme, tafsiri vipi, pinda historia na nukuu maandiko kwa namna unavyotaka ukweli mmoja unabaki: Yesu Kristo ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, Mwana wa Mungu aliyejifunua kwa mwili, aliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, akafufuka siku ya tatu, na yu hai milele! Hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu tupate kuokolewa kwalo ila jina lake (Matendo 4:12).

Na leo hii sauti ya Roho Mtakatifu inasema: “Usiitie moyo wako ugumu.” Kristo hakuja kuanzisha siasa, Kristo hakuja kubuni dini, Kristo hakuja kwa hila za Paulo, Kristo alikuja kwa damu yake mwenyewe. Na damu hiyo inamlilia kila mmoja: wokovu, msamaha, uzima wa milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…