Pawepo na uwezekano wa Marais wastaafu kugombea kiti cha Urais kwa mara nyingine baada ya miaka 10

Pawepo na uwezekano wa Marais wastaafu kugombea kiti cha Urais kwa mara nyingine baada ya miaka 10

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,794
Reaction score
9,075
Mimi nimejaribu kusoma katiba ya JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kuanzia

SURA YA PILI
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA RAIS

Rais wa Jamhuri ya Muungano

33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Nakatika kipengele hiki cha sheria
Rais wa Jamhuri ya Muungano
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9

Sikuona sehemu inayoeleza Rais hataruhusiwa kugombea tena bada kumaliza muda wake wa miaka 10 ya kuwa Rais. Mimi nataka nipeleke pingamizi mahakamani pawepo na uwezekano wa Marais wastaafu waweze kugombea kiti cha uras kwa mara nyingine endapo Rais ataona anuwezo kiafya kifikra kuweza kusimamia majukumu ya urais.

Tunaweza kufanya hivyo kama baadhi ya nchi zimekuwa zikifanya siyo lazima tukumbatie mifumo ya waingereza kwani kufanya hivyo tunabaki paler pale hata mahali Rais alikuwa ameishapafikisha unakuta anaondoka lakini kama angekuwa na uwezo wakugombea tena hii ingeleta ufanisi katika nchi yetu.

Pia unakuta Rais anajifunza kutokana na makosa aliyoyafanya hivyo anaona akipata tena anaweza kurekebisha mahali alipokosea!Sasa umefika wakati wakufanya hivyo na kama haimo kwenye katiba iwekwe kawasasa pia lazima tuwe na sheria ya kuwajibika kwa maana Rais aondolewe kinga akifanya makosa ashitakiwe bila kuangalia kosa kalifanya muda gani,endapo kosa limefanyika akiwa katika madaraka na nila kizembe awajibishwe na sheria au ajiudhuru.

Ni mawazo binafsi.
 
Kuboresha vifungu vyenye maslahi kwa taifa hamtaki kazi kujipendekeza tu.
 
kirusi hicho kinaitwa UCHU WA MADARAKA na ndicho kinawamaliza WAAFRIKA wenzetu hiki tunacho kipandikiza sasa kitakuja kutumaliza tukemee hili pepo mapema TANZANIA isije kuingiza doa la damu kwenye bendera, kama yatatumika mabavu ama njia yeyote ya nguvu kupitisha hilo ataweza ila huko tuendako kutaleta majibu mabaya sana kama tunayo yaona kwenye ma tv kwa wenzetu ndio yatakayo tukuta
 
Tunampa Rais Magufuli miak 10 mingine, wakituuliza, tunawaambia watwambie nini kilitokea kwenye uraisi wa Marekani March 4, 1933 – April 12, 1945 . na kwa nini sisi tusifanye the same?

Kwa wale wasio jua historia ni kuwa traditionaly maraisi wa Marekani hutawala miaka 4, kipindi cha kwanza, na wengi tu wameshindwa ku le-elected miaka 4 ya kipindi cha pili, ila kuna mbabe mmoja
Franklin D. Roosevelt
Ndo Rais pekee alie tawala vipindi vitatu, na mauti yakamchukua wakati keshachagulia kwenda kipindi cha nne, yaani inshort jamaa likuwa anatawala miaka 16 hivi hivi.

Franklin D. Roosevelt Ni Nani?

Ni yule raisi alie watoa Wamarekani kwenye Great Depression, ndie alie ongoza Marekani katika vita ya 2 ya dunia,

Ni rais alieweka misingi ambayo leo hii Marekani ni Marekani kwa mchango wake mkubwa.

Kama hata Wamarekani, wanajua kuwa ukimpata mtu kama Franklin D. Roosevelt inabidi umpe muda zaidi, sisi ni nani? Tumuachie Magufuli 2025. Et Demokrasia, Mnaijua Demokrasia nyie? Demokrasia ni kusikiliza kile mtaa unataka, na sasa raia wachini wanamtaka Magufuli hadi 2040 kama Mungu atamuacha awe hai.

Moja kati ya Upuuzi unaoendelea nchi nyingi za Kiafrika, ni kuwasikiliza wanachosema wazungu leo, Kumbe hatupaswi kuwasikiliza wanachosema leo, tunapaswa kuwasikiliza walichosema walipokuwa kama sisi. Walipkuwa kama sisi, wakati bado wanahangaika kujenga uchumi wa nchi, waliruhusu haya mambo, wewe unakuja kuwasikiliza leo, ni kama vile kutumia notisi za economics za masters kujiandaa na mtihani wa form 6.
 
. Ndo nyie aina ya watu mnaombaga yesu arudi Leo, pindi tu mkiwa na shida zikiisha mnaomba siku zisogee sogee.
 
nini kilimuua!!!?
 
Back
Top Bottom