Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habarzi za Wakati huu;
Wakati fulani nilipitia kipindi kigumu sana kibiashara na kujikuta ninayumba sana katika biashara na katika maisha kwa ujumla.Ndani ya kipindi kifupi sana nilipata hasara ya zaidi ya TZS 20M na kupoteza biashara yenye thamani ya zaidi ya milioni 80 huku nikiharibu mahusiano mazuri niliyokuwa nimejenga na wateja wangu.Chanzo kilikuwa ni nini?
Nilikuwa na bidii sana,kujituma na ubunifu katika kazi na mara zote nilizingatia ubora wa kazi na kumridhisha mteja.Nilikuwa na timu ndogo ambayo ilikuwa makini na yenye kujituma sana na kwa hakika tulikuwa na biashara ambayo ilikuwa na inakua kwa kasi sana.Mimi kama mbeba maono nilkuwa nafurahia mafanikio ya biashara ila nilisahau jambo moja la muhimu sana.SIKUWA NAJILIPA MSHAHARA.Nilikuwa nawalipa wenzagu mshahara ila sikuwa najilipa mimi.Ndio nilikuwa natumia mapato ya biashara/faida kwa matumizi yangu binafsi lakini ukweli ni kwamba sikuwa najilipa.Baada ya Biashara ya kuyumba na mimi kupata muda wa kutafakari sababu ya kuyumba kwa biashara pamoja na mambo mengine ni swala la mimi kutokujilipa.Kwa kutokujilipa nilishindwa kutambua thamani yangu na mchango wangu katika biashara.Kwa kutokujilipa nilishindwa kutambua iwapo biashara yangu ilikuwa na tija.Niliridhika na vijisenti nilivokuwa natoa hapa na pale kusukuma mambo yangu mengine mpaka siko biashara ilipokoma kabisa ndo nikatambua kwamba nilikuwa nakosea.
Unapofanya Biashara yoyte ile,iwe ndogo au kubwa ni lazima UJILIPE WEWE KWANZA(PAY YOURSELF FIRST).Faida za kujilipa ni nyingi sana hasa ukizingatia kwamba unatumia muda na nguvu zako kufanya kazi na kuzalisha kwa nini usijilipe wewe kwanza?
Jitendee wewe kama vile ambavyo ungependa wengine wakutendee.Iwapo ungekuwa unamfanyia mtu kazi ungetaka akulipe tena malipo halali sasa kwa nini unaona uchungu kujilipa mwenyewe?Kwa nini unaogopa kujilipa mwenyewe?Je unajua kwamba KUjilipa wewe kutakufanya uwe na hamasa zaidi ya kufanya kazi kuliko uspojilipa?Je unajua kwamba kujilipa kutakufanya uwe na nidhamu ya matumizi kuliko usipojilipa?Je unajua kwamba kujilipa kutakufanya uelewe thamni na uwezo wa biashara yako?Je unajua kwama ukijilipa unaongeza uwezo wako wa kukuza biashara yako na kuiongezea tija?
Ili uweze kujilipa lazima uweke bajeti ya matumizi,Je Utajilipa kiasi gani?
Tujadili.Tujengane.
Kwa wale ambao watakuwa interested kuwa seheme MVP(Managed Ventures Program) ambayo ni Pilot Scheme Unaweza kutuma Email kwenda masokotz@yahoo.com na utatumiwa maelezo zaidi kuhusu MVP.Zipo nafasi 15 tu za kuwa sehemu ya MVP kwa wale ambao tayari walishaomba kujiunga tutawajulisha juu ya hatua inayofuata.
Nawatakieni Kila la heri katika jitihada zenu