Pazia la Tanzania Premier League 'TPL' kufungwa leo Viwanja Tofauti, Mtibwa Sugar Vs Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) kwa msimu wa 2018/2019 linatarajiwa kufungwa leo Mei 28, 2019 kwa timu zote 20 kupepetana kunako Viwanja tofauti nchini Tanzania

Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni ambao tayari ametangazwa kuwa Bingwa wa TPL, kwa mara ya pili mfululizo kwa msimu wa 2018/2019, itakuwa ugenini kukipiga na WakataMiwa, Mtibwa Sugar kuanzia saa 9:00 Alasiri kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Mechi ya Mtibwa Sugar, dhidi ya Simba SC, itakuwa sambamba na sherehe za kukabidhiwa kombe la Ligi Kuu Tanzania TPL, huku vita vikiwa kwenye michezo hii ni zile zilizo kwenye nafasi za mwisho katika msimamo wa TPL, Nani kushuka daraja kuungana na Klabu ya African Lyon? Na nani kubakia..?

Tujuzane hapa JF kwa kila ambaye yuko uwanjani katika pembe zote za Tanzania ama yupo karibu na Tv, Kumbuka mechi zitaanza saa 10:00 jioni na mechi Tano kuwa Mubashara Azam Tv.
 
Kikosi cha Simba SC kinazoanza leo
 
Mungu ibariki simba mnyama mkali kabisa msituni
Wachezaji muwape raha wana morogoro
Kukiwa na kombe uwanjani team yetu sijui tunakwama wapi Hivi karibuni

Vodacom PL. Simba Vs kagera 2018
Sportpesa Simba vs gor mahia 2018
Kagame cup. Simba Vs Azam 2018
Mapinduzi cup Simba Vs Azam 2019
 
Nawaombea Kagera Sugar wafungwe
 
Tutakuwa na kadam ka jurgen klopp, tukishinda leo, tarehe 1 liver ananyenyua kombe, tukishindwa leo, liver akinyenyua kombe basi katusafishia njia msimu ujao..

Ni imani tu!
 
Tutakuwa na kadam ka jurgen klopp, tukishinda leo, tarehe 1 liver ananyenyua kombe, tukishindwa leo, liver akinyenyua kombe basi katusafishia njia msimu ujao..

Ni imani tu!
Tuombe Leo mambo yawe mazuri Kuna raha Sana kushinda game ya mwisho huku mnabeba ndoo
 
Kange ameshafika uwanjani? maana yule jamaa simuamini.
 
Walio salama ni kumi yaani pts 47. The rest karibuni tupange matokeo tupate hela.....
 
Shadeeya ,nakusalimia kwa jina la mk14
 
FT: Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC
 
John Boco na Okwi..
Siwaoni. Kombe kabeba Captain msaidizi.
 
Yanga tunefungwa 2 na Azam. Tumewaachia tu tukiamua tunaweza kuyarudisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…