Form Five muda bado unao. Likizo yenu inaisha sijui uko mkoa gani unasomea na unakuwa likizo wapi. Ungepiga papers za kujiinua na tuitions za kukubeba kama walimu hawako vizuri sana shuleni.
Kama walimu wako poa ila wewe ndio huelewi piga disc na watu wanaojua afu kuwa na vitini vyako unavyotumia wala usichanganye materials.
Mimi nilisoma kwa Issue Boy (Josephat) Biology na Chemistry kisha Mgote Physics. Organic nilisoma ya Ngaiza imejaza kila kitu afu Inorganic nilisoma ya Issue Boy. Yani ukichanganya madesa hutoboi utachanganyikiwa. Kuna muda nilikuwa sisomi notes za mwalimu ambaye alikuwa vizuri sana kwa vile nishasoma kwingine, kwake nafanya mifano aliyotoa nikiipiga nishamuelewa, nisipoelewa najua nalag behind. Unaweza soma sana afu kumbe tactics mbovu.
Ni kawaida sana kukata tamaa ukiwa A level. Ila ni kawaida sana tena sana kupindua meza, hili wengi niliona waliweza. Jiulize una mademu, shule mnabanwa au mnazurula mitaani, unalewa au kuvuta, unashiriki makandokando kama dancing, kuwa mtumishi kupitiliza au mpira. Punguza baadhi ya vitu vinavyokula muda.
Usiwe na mkumbo wala kujilinganisha na watu kwenye kipato, uwezo kiakili, muda wa kusoma na mengine. Pia kuwa emotional stable, sio leo umeachika kwa Winnie mara Jane anakuzingua, kesho umekamatwa na simu au umetoroka ukaitwa kwa discipline master. Zoea kwenda dini ila usifie uko, kuna majinga yalikuwa yanalala kanisani eti yanalinda vyombo.
Ningeshauri mengi kama ningekuuliza kwanza afu nikajua situation. Ila hapa nimepiga kiujumla. Mimi nilikuwa na kasoro ila zilikuwa zinazidiwa na mchanganyiko wa mambo mazuri mengi.
View attachment 1744149