PCB inanisumbua naombeni ushauri

Nakumbuka mtihani wa kwanza wa A level pale tosamaganga Biology wa kwanza alikua na 17,Chemistry atleast watu walipiga C zilikuwepo ila Physics huko siongei kabisa. Lakini hili halikutukatisha tamaa wala kuwachukia walimu sababu tuliwaza tunaendaje mbele tena kama group sio mtu mmoja mmoja. Tuligundua kilitutesa matokeo ya form four tukaanza Advance tukijua tunaanzia tulipoishia form 4,tukaelewa hii ni elimu mpya na tumeanza upya ile ya O level tukaiweka chini tukaanza vyema zaidi kwa kujifunza na kuelekezana zaidi. Tunaposema kwenye makundi tunashauriana na kueleweshana, weekend refreshment muhimu nazikumbuka safari za Ipamba,Iringa mjini,Ifunda etc.
Kikubwa soma kwa malengo na chagua marafiki zako vizuri,elewa hapo umeanza upya usidanganyike na maksi za Olevel.

Mwisho wa siku future sio udaktari pekee PCB ina fursa nyingi sana sana,nimesoma PCB ila nikaenda kusoma Horticulture leo ni Business Developer wa Tanzania wa kampuni binafsi. Kikubwa soma topic ielewe tafuta past papers pitia maswali yake tu ukiona umeelewa sogea mbele.
Ukiona topic kila unavyojitahidi uielew iache soma zingine utairudia mbeleni ukiwa umecover zingine,topic ni nyingi kuliko muda ukikomaa na moja muda utakuacha
 
Pole sana kiongozi kusoma nje kwa 4m tena MD aiwezekani ata kidogo pambana urudie sem tu io mzee tumepitia uko nakaribia tunamaliza saizi .ila sikuizi walivowawekea under Nacte mnapata tabu kwa kwer
 
Kemia rahisi pambana solve sana maliza ngaiza zote then uje huku muhimbili usome pharmacy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…