PCCB Kinondoni sheria inasemaje mtumishi wa Serikali akishtakiwa "Anaendelea na kazi"?

PCCB Kinondoni sheria inasemaje mtumishi wa Serikali akishtakiwa "Anaendelea na kazi"?

Mpira wa kona

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2016
Posts
350
Reaction score
338
Juzi nilikuwa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kufuatilia taarifa mbalimbali.

Nikiwa pale nikasikia karani wa Mahakama akitaja majina Na kuelekeza kuwa waliotajwa kesi zao ziko Kwa mahakimu Kwa kutaja namba ya vyumba.Nikaamua nifuatilie kesi mojawapo iliyokuwa inaendeshwa Na Afisa wa Takukuru Wilaya ya Kinondoni dhidi ya Watumishi wa Serikali Manispaa ya Kinondoni.

Kilichonishangaza ni kuona wale Watumishi licha ya kuwa Na Kesi bado wapo Ofisini wanaendelea Na Kazi zao kama kawaida.Swali langu ni Je Mtumishi wa Serikali anapokuwa ameshtakiwa Na TAKUKURU je wakati wote wa kesi anakuwa kazini au anasimamishwa Kazi?

Na kama anasimamishwa Kazi kwanini Watumishi hao bado wako Kazi?

Ni kwanini hawajasimamishwa Kazi kama Sheria inavyotaka?
 
>>> SHERIA haizingatiwi NDIO maana MAHAKAMA ya MAFISADI ni KIINI MACHO tu >>>
 
Mkuu kwani wamethibitishwa na mahakama kama wana hatia? au ulitaka wafukuzwe kwa sababu zako ambazo mahakama hazijazithibitisha
 
Kwani kuuliza ni kosa MKUU "Shiii"? Mie nimewauliza Pccb si we we mbona una kiherehere
 
Nadhani umekurupuka swali language ni hili mtumishi wa serikali anapokuwa kashtakiwa mahakamani Na Pccb je anakuwa anaendelea Na Kazi za ofisi yake kama kawaida au anasimamishwa Kazi mpaka kesi imalizike? Neno kumfukuza linatoka wapi hapo? Mkuu usikurupuke kuchangia kama hujaelewa
 
Kumsimamisha ni maamuzi na busara za mwajiri kama anaona mtumishi anaweza kuwa tishio au kuendelea kufanya makosa mengine atamsimamisha na kumpa mshahara mzima kasoro posho,au pccb wenyewe wanaweza kujenga hoja kwa mwajiri kuwa mtuhumiwa anaweza kuharibu ushahidi akiendelea kuwa kazini basi atasimamishwa
 
Rationality ya kumsimamisha kazi mfanyakazi mwenye kesi mahakamani ni pamoja na kupungua kwa umakini kazini kunakochangiwa na msongo wa mawazo.

Taasisi nyingi za Serikali, mtuhumiwa lazima asimamiswe uchunguzi ufanyike (pia kesi kama atakua kwenye nafasi tatanishi) katika kesi hususani.
 
Back
Top Bottom