Mjukuu wa kigogo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 445
- 1,094
Hii ikufikie Boss wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (PCCB) wilaya ya Bunda mkoani Mara. Wiki hii Kuna kijana mmoja ambaye kaanzisha operation ya kupita kwa baadhi ya maduka ya wafanyabiashara na kuwaulizia kama tayari washalipa leseni za biashara au la. Inajulikana wazi wafanyabiashara wote iwe hapa Tanzania au mahali pengine duniani wana wajibu wa kulipa kodi Kwa ajili ya maendeleo ya Taifa lao.
Kijana huyu ambaye hujitambulisha kama afisa maendeleo ya jamii kata ya Bunda mjini anafanya ukaguzi pasipokuwa na kitambulisho kinachomtambulisha ofisi anayotoka na anapoulizwa na wafanyabiashara kwamba watamtambuaje kwamba yeye ni afisa maendeleo ya jamii bila kuwa na kitambulisho,anaanza kutishia na kuibua visababu vya kutishia ambayo ni kama kutoa alert kwamba watakuja kutengenezewa mizengwe ili wakione cha moto siku za baadae na kufunga biashara zao.
Lililoko nyuma ya pazia inaonekana huyu jamaa anatumiwa na baadhi ya watendaji wa kata wasio waaminifu katika kutengeneza mazingira ya rushwa kwa wafanyabiashara. Na inawezekana kabisa watu wakaanza kuundiwa mizengwe ili wafunge biashara zao. Mamlaka imfuatilie kwa kina sababu ya yeye kufanya ukaguzi pasipo kitambulisho huku akitoa vitisho anapoombwa kuonyesha kwa wafanyabiashara. Anaficha kwa sababu zipi? Na pia bado wananchi hatujaelezwa kama maafisa maendeleo ya jamii ndio wanahusika kukagua leseni za biashara.
Na kama wao ndio wahusika iweje mhusika atembee na kufanya ukaguzi bila kuwa na kitambulisho au walau kuambatana na baadhi viongozi ya viongozi wa serikali walau hata balozi, nk. Watu kama hawa wakishirikiana na watendaji wasio waaminifu wapo nchi nzima na wanasababisha wafanyabiashara wengi kufunga biashara zao na mwisho wa siku vita dhidi ya umaskini inakuwa ngumu!
NB: Inadaiwa jina la huyo mhusika ni Mapunda.