Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na. M. M. Mwanakijiji
Ukweli umebakia kuwa ukweli CCM bado inapendwa na kukubalika mijini na vijijini. Hili halina shaka. CCM kuweza kuendelea kutawala bado kupo kwa miongo kadhaa ijayo. Hilo nalo silishuku sana. Kwamba, kizazi kipya cha viongozi wa CCM kinazidi kupanda taratibu hilo nalo halina shaka.
Kwamba lengo la Chama cha Mapinduzi liko wazi kabisa kwa mtu yeyote kulielewa. Siyo lengo la kubuni, kuhisi au kulikisia. Lengo hilo kubwa limeanishwa katika Ibara ya
Hii ina maana ya kuwa CCM kama chama kinajua kabisa hakiwezi kufanya jambo lolote na hakiwezi kutekeleza sera yoyote bila kuweka kipaumbele chake sawa. Kwao kushinda uchaguzi ndio msingi wa mambo mengine yoyote na kutokana na hilo watafanya lolote wawezalo kuhakikisha wanashinda hata ikibidi kutumia njia za panya, hadaa, au mbinu za kisiasa ambazo zimekuwa zikizaa matunda. Siwalaumu kwani wanajua lengo lao la kwanza ni nini!
Tukilielewa hili tutaelewa kuwa si rahisi kuiondoa CCM madarakani au kuinyima nafasi ya kutawala. Ni sawa na jaribio la kumkamata simba mwindaji nyikani ili afugwe kwa maonesho au kujaribu kumtoa samaki majini ili umfuge kwenye chupa!
CCM haitoachia madaraka kiurahisi, haiwezi kuachia madaraka kwa sababu tungependa ifanye hivyo, na kwa haki haipaswi kuachia madaraka kwa sababu kuna watu hawaipendi, no sir! CCM kama chama cha siasa kina sababu, haki, na nia ya kung'ang'ania madarakani kwa muda mrefu na kwa mbinde au kwa upinde. Ndiyo historia ya watawala wote duniani.
Hivyo mabadiliko basi yatakuwa magumu.
Mabadiliko hayaji kiurahisi na CCM hakiwezi kutengeneza mazingira ya mabadiliko ambayo yatasababisha chenyewe kiondolewe madarakani. Kama chama kimejifunza yaliyotokea Kenya, Zambia na Malawi, kimejifunza yaliyotokea Zimbabwe na hakiko tayari kurudia makosa yale yale. CCM kitakkuwa ni chama cha wapuuzi na wajinga endapo kitasababisha na kusimamia mabadiliko ambayo yatasababisha chenyewe king'olewe na watoto wake wakae pembeni ya meza kuu ya utawala na ulaji. Hapana ma'am, CCM haiwezi kufanya hivyo hata taifa zima likiwa usingizini.
Kwa upande mwingine hata hivyo, CCM inaweza kabisa (naamini ndivyo inavyopanga) kufanya mabadiliko ya kukifanya kikae madarakani zaidi na kukubalika zaidi. Mabadiliko hayo si mengi wala si makubwa. Kinahitaji kufanya mabadiliko ya ishara na alama; mabadiliko ya picha na sauti. Mabadiliko ya nyimbo na kibwagizo. Kwa wengine mabadiliko hayo yanatosha kabisa.
Pamoja na hayo kuna mabadiliko ambayo CCM haiwezi kuepuka kufanya kwani kutofanya hivyo kunatishia uhai wa chama chenyewe. Mabadiliko haya yanategemea sana nani atashinda katika siasa za ndani za chama (intraparty politics). Katika makala yangu moja ya kesho nimetuma ujumbe wa wazi kwa kiongozi mmoja wa CCM ambaye kambi yake inaamini itashinda siasa hizi. Endapo upande wa mtu huyo utashinda, basi CCM itajikuta inalazimishwa kubadilika na kufungua uwanja wa kushindwa kwake.
Lakini ninaamini upande huo hauwezi kushinda kwani tuliyoyaona Busanda yametuma ujumbe wa wazi kuwa bado CCM inaweza kushinda bila upande huo.
Kwa wale wengine wanaotaka mabadiliko ni lazima watambue kuwa tunaweza kupoteza kita kimoja kimoja lakini tukashinda vita. Dalili za upepo bado zinaelekea upande wa mabadiliko ya kweli. Japo pole pole. Kama merikebu iendayo pole pole na kupigwa na upepo, ndivyo hivyo hivyo mabadiliko tuyatakayo yanavyokaribia. ni mabadiliko ya fikra kwanza, kabla ya mabadiliko ya kura.
Busanda, Tarime, Mbeya Vijijini, Kiteto na hadi Tunduru kote kumeonesha kuwa mabadiliko ya fikra yameanza, kama vile cheche mbugani, na kama vile manyunyu ya mvua ndivyo hivyo hivyo moto mkubwa utaanza taratibu, kama kwa ukimya huku mlio wa majani kuungua na harufu ya nyasi kupaa ndivyo itakavyokuwa.
Tusiwe na haraka wala papara; tusikate tamaa wala kujiona duni. Mabadiliko tuyakatayo yanakuja, labda pole pole sana kuliko ambavyo tungependa. Tungependa mabadiliko yawe "sasa". Tungetaka kila uchaguzi mdogo wapinzani "washinde". Tungependa kuona CCM inaumbuka na kuabika mbele ya wapiga kura. Njozi hizo mara kadhaa sasa zimezimwa kama mtu ambamizapo mbu ukutani; na kama aliyekanyaga sisimizi ndivyo matamanio hayo yamefutwa katika mioyo yetu.
Ni mwoga hata hivyo atakayekata tamaa, ni dhaifu ambaye anajisikia kushindwa, ni mwongo ambaye hauoni ukweli uliopo mbele yetu. Moto wa mabadiliko umeanza, upepo wa ushindi unavuma taratibu, na sauti za mashujaa wapambani zinasikika kwa mbali; Vinakuja, kama vile kutoka upeoni tunaweza kuona moshi wake. Vinakuja, kama king'ora cha utangulizi vinasikika; vinakuja, kama nyota ya alfajiri kumulika. Hakuna atakayaweza kuzuia, siyo CCM wala makuwadi wa ufisadi.
Yawezekana hivyo, CCM ndiyo ikawa chanzo cha mabadiliko hayo. Yawezekana CCM ikawa ndilo tumaini la mwisho la vita dhidi ya ufisadi, yawezekana CCM ikawa ile merikebu tuitakayo, sitoshangaa. Nimekulia ndani ya CCM, nimejifunza itikadi yake, naijua misingi yake, na naijua vyema kuweza kuamini, kuwa yawezekana kabisa mabadiliko tuyatakayo yataletwa na CCM.
Nafahamu hiyo ni orodha ya "yawezekanayo". Lakini, pia yawezekana kabisa kuwa CCM ndiyo kizuizi kikubwa cha mabadiliko hayo. Jukumu letu basi ni kutambua kipi ni kipi na kukifuatilia kwa nguvu zote.
Binafsi naamini mabadiliko ya kweli yatatoka na yataletwa na Watanzania wenyewe. Yataletwa kwa machozi na kupolekewa kwa kicheko. Bado hatujalia vya kutosha ingawa tunataka kucheka sana. Bado hatujachubuka miguu kwa kutembea na kuota malengelenge kwa kukimbia. Bado Watanzania hawajaonja uchungu wa utawala wa kifisadi. Tunaishi katika ulimwengu wa kufikirika. Bado hatujakasirika vya kutosha (mabadiliko yote ya kweli asili yake ni hasira!). Bado hatujadhalilika vya kutosha.
Tusikate tamaa, tusipepese macho, na tusirudi nyuma kwa kujisalimisha isipokuwa kwa kujipanga tena. CCM wataendelea kusonga mbele kama mashujaa walioshinda, na wanastahili kusonga mbele. Wataendelea kusogea zaidi hadi watufikishe mahali ambapo hatuwezi kurudi nyuma tena. Hapo ndipo songombingo litakapoanza, hapo ndipo sauti za wapiganaji wa kweli na mashujaa wasiosalimu amri zitakaposikika, kwani ni hapo ndipo tutajua kuwa tunachopigania ni zaidi ya sisi kusimama, tutakuwa tunapigania uhai wetu na urithi wetu.
Mapambano haya siyo sawa na mbio za mita 100; hii ni marathoni. Si mapambano yanayofikiria 2010 au 2015, ni mapambano yanayoangalia 2020 na baadaye. Kwa wenye pumzi ndogo ni bora kukaa pembeni; wenye haraka ni bora wakafanye jambo jingine, na wenye pupa ni bora watulie watazame.
Kesho, ni mwanzo tu! Inua kichwa chako, simama wima, tazama mbele na acha kumung'unya maneno. Jifunge mkando wako. Kuna mapambano mbele. Huwezi, rudi mstari wa nyuma, umeshindwa kaa pembeni, hutaki jiondoe. Vinginevyo. Aluta continua!
Mwanzo tu huu.. bado mapemaaaa!!
NB: Gazeti lolote linaweza kutumia makala hii.

Hilo ndilo lengo la kwanza la CCM kwani kutoka hapo malengo mengine yanafuatia. Kwa kulinganisha hata hivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeyagawa madhumuni yake sehemu kubwa tatu (ya kisiasa, ya kiuchumi na kijamii). Katika madhumuni ya kisiasa yapatayo 6 hakuna lengo la "kushinda uchaguzi mkuu au wa serikali za mitaa". Hili ni muhimu kwani malengo mengine yote yanategemea kwa chama kuwa madarakani!" 5(1) Kwa hiyo Malengo na Madhumuni ya CCM
yatakuwa yafuatayo:-
(1) Kushinda katika Uchaguzi wa Serikali Kuu
na Serikali za Mitaa Tanzania Bara na
Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali
Kuu na Serikali za Mitaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

Last edited: