Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kutokana na ongezeko kubwa la viwanda Tanganyika, mahitaji ya malighafi nayo yameongezeka kwa kiasi kikubwa sana. Kuna baadhi ya malighafi ambazo zamani hazikuwa na thamani yoyote. Ni aidha ziligawiwa bure, zilitupwa, au ziliuzwa kwa bei rahisi.
Leo twende na hii malighafi ya oil iliyotumika maarufu kama oil chafu. Oil chafu zina aina zake, nitazitaja kwa makundi yake:
Zilizo Maarufu
Zisizotambulika Sana
Nitaendelea...
Leo twende na hii malighafi ya oil iliyotumika maarufu kama oil chafu. Oil chafu zina aina zake, nitazitaja kwa makundi yake:
Zilizo Maarufu
- Oil zilizotumika kutoka kwenye injini za magari, mitambo, na mashine mbalimbali.
- Hydraulic zilizotumika kutoka kwenye gearbox za magari, mitambo, na mashine mbalimbali.
Zisizotambulika Sana
- Tope toka kwenye matank makubwa ya kuhifadhia mafuta.
- Mabaki ya mafuta toka kwenye meli zinazoleta mafuta.
- Mabwawa ya kuhifadhia uchafu unaosafishwa (sledge) kutoka kwenye matank na hifadhi za mafuta.
- Mafuta ghafi.
- B.O (Base Oil): Hii ni oil maalum inayotumika kwenye bahari kuu kufukuza maji kwenye mwamba wakati wa kuchoronga kwa ajili ya utafiti wa gesi asilia.
- O.B.M (Oil Base Mud): Hii haina tofauti na B.O ila hii inakuwa imechanganyika na tope zaidi kuliko B.O.
- Condensate: Haya ni mabaki ya gesi wakati wa kuchuja gesi asilia.
Nitaendelea...