Deejay eXii
Member
- Feb 22, 2025
- 33
- 37
Katika mambo yanayozua mijadala sana hivi karibuni hasa ndani ya jamii ya watu weupe ndani ya nchi ya marekani ni jinsi ambavyo wanaitizama jamii ya weusi.
Jamii ya watu weusi imekuwa kila sehemu katika nyanja tofauti tofauti. Peacock, Netflix wamekuwa wakitoa filamu nyingi sana kila mwaka na katika hali ya kushangaza watu weusi wanaonekana kwa wingi katika filamu hizi, ama wameamua tu kuamka na kuchangamkia fursa.
Hivi majuzi mmiliki wa mtandao wa X alipost picha yenye chenga nyeusi kisha kuandika chini yake 'by Netflix' na chapisho hilo lilishambuliwa kweli kweli na wazungu wakijaribu kuelezea mitazamo yao kuhusu watu wenye asilimia 17 tu ndani ya marekani lakini ni kama wao ndio wengi ndani ya nchi hiyo.
Ni nini kinawakuta wamarekani hao, je ni kwamba wao weupe hawapendi kujumuika ama kujichanganya kama ilivyo kwa jamii hii ya weusi...!!!?.
Tuachane na mambo ya hao jamaa.
Ni serie gani umetazama katika hizi...!?. Anyway kama ujatizama hizi fanya uanze mdogomdogo humu kwenye haya madude kuna michoro kibao ya kimaisha. Niko season ya 5 kwenye All American, wikendi ijayo sitaki mambo mengi mahindi yaPopcorn ndoo ndogo nakaanga mwenyewe.