Peana Mikono na Shetani: Historia na uzoefu unaomiumiza sana toka kwa Romeo Dallaire

Peana Mikono na Shetani: Historia na uzoefu unaomiumiza sana toka kwa Romeo Dallaire

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Moyo wangu umejawa na simanzi, macho yamefunga kwa huzuni, uso umesawajika kwa haya ninayoyasoma yaliyotendwa na binadamu kwa binadamu wenzao.

Romeo Dallaire ameelezea mambo kwa mtazamo wake. Mengi ya mambo aliyoyaandika nmeyasoma pia toka kwa waandishi wengine na wana JamiiForums pia humu.

Ntaleta summary tuweze jadiliana na pengine kujifunza kitu flani. Ingawa yameongelewa sana humu ndani, lakini ngependa kufahamu tumejifunza nini.na nini hatma ya siasa zinazoendelea sasa Rwanda ukilinganisha na hayo yaliyotokea hapo mwanzo mpaka kufika hapa.

Inaumiza sana. Inasikitisha sana. Inahuzunisha sana. Inafifisha moyo. Afrika, laiti ungelijua yale yakupasayo kutenda.

Screenshot_20200613-204755~2.png
 
Kitabu chochote kuhusiana na Rwanda genocide ambacho kinaongelea events za April mpaka july 1994 pekee yaani kinachoitwa ''siku 100 za mauaji'' huku zikipuuzia matukio yote ya baada ya July 1994 hadi kuendelea August 1998 na kuishia 2003 basi kitabu hiko ni propaganda tu za magharibi.

Mfano huyo jamaa analalamika kwanini marekani ilikataa kutuma jeshi ilihali ilikubali kudhamini makambi ya wakimbizi huko DRC!!

Sasa kwa mtu asiyefuatilia siasa za ukanda huu ataona jamaa kaongea hoja ila ukweli ni kwamba mauaji ya kimbari mengi zaidi yamefanyika kuanzia july 1994 na yakaisha 2003 hasa Kongo ya mashariki ambapo ndio makambi ya wakimbizi wengi yapo huko.

Rwanda walikufa watu takriban laki 8 ila kule kongo ya mashariki vifo vya wanyarwanda na waCongo ni zaidi ya million 4!! Sasa je ni wapi ilipaswa nguvu iwekwe if at all hoja yake ya marekani kutotuma jeshi kumaliza vita ndio ilimshangaza.

Mie ningeshauri kwa wanaotaka kujua zaidi kuhusiana na ukweli wa genocide wasome vitabu vifuatavyo.

Africa's world war cha Gerard prunier

Great lakes conflagration cha Tom cooper

The Great Africa's war cha Philip Rentyjens

Maana ndio vimetoa picha nzima kuanzia Rwanda kabla na baada ya July 1994!! Tupuuze hiki kitabu cha huyu pandikizi.

Cc Proved mtu chake
 
Nadhani katika hili kila mtu asomee anachotaka kusoma then atoe maoni yake. Hakuna kitabu kitakachokuwa bora kuliko kingine sababu vyote vimeandikwa na binadamu. Na siku zote binadamu hawezi hukumu kiusahihi kwa asilimia 100.

So kama tutaamua kujadiliana tujadiliane kwa mitazamo kutoka kwa watu tofauti tofauti.
 
Mkuu huwa nakuheshimu sana na sina nia ya kudiscredit uzi wako lakini nadhani ili tufanye analysis nzuri ni bora kusoma source nyingi kwa case moja ili upate mtazamo tofauti kwa upana.

Ila kma mtu akisoma hiki tu basi ataona upande mmoja tu wa story hivyo kukwepa ukweli wa upande wa pili.

Ni maoni tu lkn
 
Nakushukuru Mkuu. Nami nakurudishia heshima hiyo. Nmekuelewa. Kiuhalisia inapaswa tusome mawazo ya watu mbalimbali halafu tufanye analysis. Baada ya kumaliza hiki then nitaanza hivyo ulivyo shauri. Ili baadaye tuweze kujadiliana kulingana na tulichosoma.

Romeo namwelewa lawama zake kwa sababu ya kile alichoona kwa macho yake na alichokuwa akikiongea kwa wahusika.nliangalia hata documentary yake akiwa amerudi Rwanda miaka 10 baadaye. The man ni kweli ameathirika sana. Mimi binafsi zaidi ya mara 5 nmeota haya NINAYOYASOMA. najiuliza yeye aliyeshuhudia?

Lakini nashindwa sana kuwalaumu wazungu. Why tuwalaumu wazungu? Wana makosa yao sikatai.but kuendelea kuwalaumu wazungu ni kujishusha sana na kuwapa mawazo kuwa sisi ni hatujiwezi.

Waafrika walikuwa wapi? Mataifa ya afrika yalikuwa wapi?kwa nini amani ya nchi zetu za kiafrika ambazo siku zote tunalaumu zilitengenishwa na mipaka ya wazungu tushindwe ilinda? Hili linaniumiza zaidi.

Back
Top Bottom