Peke yako hauwezi

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Huwezi kusimama peke yako na kudumu kwenye mafanikio makubwa kwa muda mrefu bila kuwa na watu Pamoja na mifumo iyakayokubeba na kukusaidia kupanuka.

Unahitaji msaada kwenye maeneo haya:

1. Msaada wa KITAALAMU:
Kuna maeneo ambayo hujafuzu wala huna maarifa na ujuzi lakini bado unayahitaji kwa ajili ya mafanikio yako. Kwa mfano, unahitaji huduma ya kisheria, au usimamizi wa mahesabu kama ni mfanyabiashara. Ukifanya mwenyewe utaishia kwenye matokeo madogo. Lakini ukiwapa nafasi wabobezi, watakusaidia kufika mbali zaidi.

Gharama unayowalipa haifikii ukubwa wa matokeo unayopata. Ni vema kuwatumia kwa faida yenu nyote kwa pamoja.

2. Msaada wa KIUTENDAJI
Unahitaji watendaji kwenye kitu chako unachofanya. Hawa ni watu wanaotekeleza maono yako kwa maelekezo unayowapa. Ni watu wa muhimu sana kwa sababu peke yako huwezi kuwahudumia watu wote. Wasaidizi wako watakusaidia kufika pale ambapo muda, uwezo na nafasi havikuruhusu kufika.

3. Msaada KIUWAJIBIKAJI
Matokeo makubwa yanamilikiwa na watu wanaowajibika. Sio mara zote inakuwa rahisi kuwa na nidhamu ya kuwajibika; unahitaji watu watakaokusimamia, kukupima na kukukumbusha kuhusu wajibu wako kwenye mipango, maono na malengo uliyojiwekea ndani ya muda na wakati.

Hakikisha unaweka mifumo itakayokusaidia kusimama kwa kila hatua ya maendeleo unayopiga.

__________
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…