Pele na Santos wageni wa Yanga, kisha mgogolo mkubwa mwaka 1976.

Pele na Santos wageni wa Yanga, kisha mgogolo mkubwa mwaka 1976.

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,697
Kuna mwana jamvi kaulizia histolia ya kitu hicho juu katika jukwaa linguine, mimi ninafahamu haya:-
Mwaka 1975 Yanga enzi hizo iko chini ya Mzee Mangala Tabu Mangala kama mwenyekiti na Johnson Mbwambo mwajiliwa wa Tanzania breweries alikuwa ndiye meneja wa Yanga na Shiraz Sharif kama mfadhili mkuu . Hao wote walibuni project ya kuialika timu ya Santos ya Brazil ambayo ndiyo Pele alikuwa akichezea, deal hilo liliratibiwa na Meneja Mbwambo ambae alienda Brazil kufunga mkataba, katika makubaliano ilikuwa timu ya Santos ije bongo kama wa wageni wa Yanga but not without king Pele, ilikuwa katika ziala hiyo na Pele awemo na si vinginevyo.


Sasa kilichofuata baada ya wakati kuwadia mke wa King Pele akajifungua mtoto, kwa mantiki hiyo ilibidi King Pele awe karibu na mkewe kwa hiyo angekosekana katika safari , automatically deal likafa au mipango ikaharibika na ziala ikafutwa . Siyo serikali alifuta ziara hiyo kama mdau alivyosema ni Yanga wenyewe walighaili. Walikuwa wametengeneza Kanga nzuri za rangi ya kijani na njao zenye maneno PELE NA SANTOS WAGENI WA YANGA, mpaka hivi leo baadhi ya akina mama wanazo wamezitunza mfano Mama Matuga wa Mpwapwa anazo.


Kuhusu mgogolo mkubwa wa Yanga mwaka 1976, ili uelewe vizuri kuhusu mgogoro ule inabidi kwanza ujue background information. Enzi hizo ushabiki wa Simba na Yanga haukuwa kama ulivyo hivi sasa, nyakati hizo ulikuwa ni ushabiki wa kufa mtu, ulikuwa ushabiki kweli kweli wa kutoka moyoni watu walikuwa teyari kufa kwa ajili ya hizo team,pamoja na kocha mashabiki na viongozi walikuwa na uwezo wa kupanga team itakayocheza walikuwa na uwezo wa kumwingilia kocha, kwa ujumla timu hizo zilikuwa na ushabiki mkongwe. Mchezaji wa yanga alikuwa hawezi kwenda Simba and visa versa , ilikuwa balaa Siku za mechi ya Simba na Yanga mashabiki walikuwa wanaanza kuingia uwanjani saa mbili asubuhi na mechi inaanza saa 10.30 na walikuwa wakitokea pande zozote afrika mashariki, siku ya mechi hiyo ilikuwa siku ya pekee kabisa.


Sasa Yanga mwaka 1974 walifanya ziara Brazil huko walimpata kocha mkongoman akiitwa Tambwe Leya, kuona hivyo Simba nao wakafruke kumpata kocha Mghana aliyeitwa Nabi Kamala. Mwaka 1975 Yanga iliwakilisha Taifa kwenye mashindano ya vilabu bingwa Afrika walipangiwa kucheza na Enugu rangers ya Nigeria ,mechi ya kwanza Nigeria walitoka sare ya bila bila, mechi ya pili Dar wakatoka sare ya 1.1 Yanga wakatolewa kwa goli la ugenini. Kocha akawatuhumu wachezaji Fulani kwamba wamehujumu timu kwa kukosa kujituma basi akawashusha team B , kati ya hao alikuwepo Sunday Manara ikumbukwe kwamba Sunday Manara alikuwa kama mfalme na ufalme wake Tambwe Leya akaamuwa kumpiga chini kama nilivyosema hapo juu kocha alikuwa hana uwezo wa kuacha kumpanga Sunay Manara enzi hizo kumweka benchi Sunday Manara ni kwamba kocha hujipendi, kuanzia hapo ulizuka mgogolo mkubwa uliopelekekea wachezaji kufukuzwa . Mgogolo ukawa mkubwa mpaka inchi ikatingishika, serikali kuona hivyo ikaingilia kati amani ilitoweka kisa nini kocha kawapiga benchi wachezaji wa Yanga basi ikaamuru kocha afukuzwe akamponza na wa Simba naye afukuzwa.


Ndicho ninachokumbuka katika histolia , nawasilisha.
 
kuna mwana jamvi kaulizia histolia ya kitu hicho juu katika jukwaa linguine, mimi ninafahamu haya:-
mwaka 1975 yanga enzi hizo iko chini ya mzee mangala tabu mangala kama mwenyekiti na johnson mbwambo mwajiliwa wa tanzania breweries alikuwa ndiye meneja wa yanga na shiraz sharif kama mfadhili mkuu . Hao wote walibuni project ya kuialika timu ya santos ya brazil ambayo ndiyo pele alikuwa akichezea, deal hilo liliratibiwa na meneja mbwambo ambae alienda brazil kufunga mkataba, katika makubaliano ilikuwa timu ya santos ije bongo kama wa wageni wa yanga but not without king pele, ilikuwa katika ziala hiyo na pele awemo na si vinginevyo.


Sasa kilichofuata baada ya wakati kuwadia mke wa king pele akajifungua mtoto, kwa mantiki hiyo ilibidi king pele awe karibu na mkewe kwa hiyo angekosekana katika safari , automatically deal likafa au mipango ikaharibika na ziala ikafutwa . Siyo serikali alifuta ziara hiyo kama mdau alivyosema ni yanga wenyewe walighaili. Walikuwa wametengeneza kanga nzuri za rangi ya kijani na njao zenye maneno pele na santos wageni wa yanga, mpaka hivi leo baadhi ya akina mama wanazo wamezitunza mfano mama matuga wa mpwapwa anazo.


Kuhusu mgogolo mkubwa wa yanga mwaka 1976, ili uelewe vizuri kuhusu mgogoro ule inabidi kwanza ujue background information. Enzi hizo ushabiki wa simba na yanga haukuwa kama ulivyo hivi sasa, nyakati hizo ulikuwa ni ushabiki wa kufa mtu, ulikuwa ushabiki kweli kweli wa kutoka moyoni watu walikuwa teyari kufa kwa ajili ya hizo team,pamoja na kocha mashabiki na viongozi walikuwa na uwezo wa kupanga team itakayocheza walikuwa na uwezo wa kumwingilia kocha, kwa ujumla timu hizo zilikuwa na ushabiki mkongwe. Mchezaji wa yanga alikuwa hawezi kwenda simba and visa versa , ilikuwa balaa siku za mechi ya simba na yanga mashabiki walikuwa wanaanza kuingia uwanjani saa mbili asubuhi na mechi inaanza saa 10.30 na walikuwa wakitokea pande zozote afrika mashariki, siku ya mechi hiyo ilikuwa siku ya pekee kabisa.


Sasa yanga mwaka 1974 walifanya ziara brazil huko walimpata kocha mkongoman akiitwa tambwe leya, kuona hivyo simba nao wakafruke kumpata kocha mghana aliyeitwa nabi kamala. Mwaka 1975 yanga iliwakilisha taifa kwenye mashindano ya vilabu bingwa afrika walipangiwa kucheza na enugu rangers ya nigeria ,mechi ya kwanza nigeria walitoka sare ya bila bila, mechi ya pili dar wakatoka sare ya 1.1 yanga wakatolewa kwa goli la ugenini. Kocha akawatuhumu wachezaji fulani kwamba wamehujumu timu kwa kukosa kujituma basi akawashusha team b , kati ya hao alikuwepo sunday manara ikumbukwe kwamba sunday manara alikuwa kama mfalme na ufalme wake tambwe leya akaamuwa kumpiga chini kama nilivyosema hapo juu kocha alikuwa hana uwezo wa kuacha kumpanga sunay manara enzi hizo kumweka benchi sunday manara ni kwamba kocha hujipendi, kuanzia hapo ulizuka mgogolo mkubwa uliopelekekea wachezaji kufukuzwa . Mgogolo ukawa mkubwa mpaka inchi ikatingishika, serikali kuona hivyo ikaingilia kati amani ilitoweka kisa nini kocha kawapiga benchi wachezaji wa yanga basi ikaamuru kocha afukuzwe akamponza na wa simba naye afukuzwa.


Ndicho ninachokumbuka katika histolia , nawasilisha.
asante kwa yote.ila nabi camara alikuwa ni raia wa guinea na sio ghana.
 
Back
Top Bottom