Pelvic Inflammatory Disease (PID)

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
PELVIC INFLAMATORY DISEASE (P,ID),Ni maambukizi katika via vya uzazi wa mwanamke au mfumo wa uzazi wa mwanamke,,kwa kawaida maambukizi haya ynahusiana na mji wa mimba (uterus,shingo ya kizazi) (cervix,( fallopian tubes Mirija ya uzazi ya mwanamke ) na sehemu yanapozalishwa mayai haya ( ovarie).

JE NI SABABU GANI AU VYANZO VYA TATIZO HILI AU UGONJWA HUU WA P,I,D

UGONJWA HUU UNASABABISHWA NA BACTERIA WA MAGONJWA YA ZINAA HUSUSANI GONORRHEA NA CHYLMIDIA

NI JINSI GANI MWANAMKE ANAWEZA PATA UGONJWA HUU SASA

• Kupitia ngono zembe (magonjwa ya zinaa kama kaswende na kisonono)

• Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja

• Kufanya mapenzi bila kutumia kinga (condom)

• Kupitia kunyonywa uke mara kwa mara

• Kuweka vitu ukeni ili kuufanya uke ubane au upendeze kwa mpenzi wako

• Utoaji wa mimba mara kwa mara ,,halafu kukosa usafishaji mzuri baada ya kutoa

• Kupitia njia ya kujifungua kwa njia za kienyeji hasa kwa wakunga kama hawatakua makini

• Kutumia madawa na njia za kuzuia mimba kama vijiti sindano n.k

• Kupitia u,t,i na fungus sugu

• Kutozingatia usafi wako binafsi

DALILI ZA UGONJWA HUU WA P.I.D
Mwanamke atagundulika kuwa na tatizo la p,i,d kama atakuwa na dalili zifuatazo

• Maumivu makali ya tumbo hasa chini ya kitovu

• Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya wenye rangi ya maziwa mgando,kijani au njano

• Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa (kujamiana)

• Kutokwa na damu wakati wa kujamiana

• Kuumwa mgongo mara kwa mara

• Kutokwa na usaha ukeni wakati mwingine

• Kupata maumivu wakati wa kukojoa.

MADHARA GANI HUMPATA MWANAMKE MWENYE UGONJWA HUU WA P.I.D
Kama mwanamke atapatwa na gonjwa hili la p,i,d akashindwa kutibiwa mapema, Madhara yafuatayo yanaweza kumtokea

• Kupata tatizo la hormone imbalance (mvurugiko wa hormone)

• Mirija ya uzazi itaziba na hivyo kushindwa kupitisha mayai yaliyopevuka ili kututubishwa

• Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa sababu ya hormone imbalance

• Kuwa na uke mkavu mara kwa mara

• Mzunguko wa hedhi (period) kubadilika mara kwa mara

• Wakati mwingine kukosa period kwa muda mrefu

• Kupata kansa ya shingo ya kizazi kutokana na kushambuliwa na bacteria

• Mimba kutungwa nje ya kizazi
 
Hili gonjwa lina tiba kweli? Kuna dada mmoja ananiambiaga linamsumbua sana pia kuna mwingine hapa nae ivoivo ametumia dawa na dawa za hospital lakini wapi..
 
Hili gonjwa lina tiba kweli? Kuna dada mmoja ananiambiaga linamsumbua sana pia kuna mwingine hapa nae ivoivo ametumia dawa na dawa za hospital lakini wapi..
Dawa zipo hasa akitembelea vituo vya Afya na kupata vipimo.
 
Je matumizi ya kondomu kwa muda mrefu yanaweza kuchangia hilo tatizo? Kwani Kuna wanandoa mmoja ni positive na mwingine negative na huyo positive amekutwa na hilo tatizo. Na je vipimo vyake vinahusisha Daktari kuingiza mkono ukeni na kuunusa?
 
Kuna visababishi vingi vya ugonjwa huu hivyo mtu mwenye ugonjwa huu huenda amepata toka chanzo kingine.
Na ugonjwa huu haupimwi kwa kunusa bali bali dakitari anaweza tumia mbinu hii kujua kama muhusika anaugonjwa au lah!
Ila vipimo hutumika kugundua ugonjwa husika.
 
Hili gonjwa lina tiba kweli? Kuna dada mmoja ananiambiaga linamsumbua sana pia kuna mwingine hapa nae ivoivo ametumia dawa na dawa za hospital lakini wapi..
Tiba ipo wasiliana nasi kwa namba 0678211747. Tunatoa huduma mikoa yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…