Pemba: Karafuu ya wiza yakamatwa, waliotoa taarifa watapewa gawio

Pemba: Karafuu ya wiza yakamatwa, waliotoa taarifa watapewa gawio

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Karafuu ya magendo yakamatwa

Magunia 30 ya karafuu yaliyokuwa yamefichwa katika Kisiwa cha Funzi wilayani Wete, Kaskazini Pemba, ili kusafirishwa kwenda nje ya nchi kwa njia ya magendo, yamekamatwa na kikosi maalumu cha kuzuia magendo (KMKM), kamandi ya pemba.

Akizungumza na askari wa kikosi cha KMKM makao makuu Pemba, mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman, amesema serikali inaridhishwa na utendaji kazi wa kikosi hicho na kuwataka kuendelea kudhibiti biashara ya magendo, ili wahusika wapatikane na kuchukuliwa hatua.

Aidha, mkuu huyo wa mkoa, ameagiza karafuu zilizokamatwa ziuzwe ili wahusika waliotoa taarifa wapatiwe mgawo.

Awali, Kaimu Kamanda wa KMKM, Omar Ali Mussa, amesema karafuu hizo zimekamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
 
Back
Top Bottom