Pemba ni sehemu ya Tanzania, kikinuka huko kimenuka Tanzania nzima

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Kamanda Siro alisema tume inawasababishia na kuwapa wakati mgumu.

WaTanzania sasa tunaelekea kule ambako vyombo vya ulinzi huenda mwisho wake vikaungana na wananchi, jambo ambalo limeonekana nchi nyingi, haiwezekani utumie vyombo vya ulinzi kuteketeza wananchi, wananchi ambao ndio wanaounda vyombo hivyo na kuvifanya viwepo kwa ndugu na jamaa zao na kodi wanazolipa.

Ipo limiti ya vyombo hivyo kufanya kazi kwenye nchi inayoongozwa kiraia kutokana na ridhaa za watu, leo hii CCM inafanya mambo kihuni na kama haitoshi inavihusisha vyombo hivyo pasina sababu ya msingi au yenye uzito, kama hapa tulipo huu si wakati wa kutumia vyombo hivyo, CCM inavitumia bila ya aibu na kuwatishia hata kuwafuta kazi wasipotimiza utumwa wa udhalilishaji. Vyombo hivi inabidi vijitathmini vinafanya kazi kwa ajili ya CCM au serikali na wananchi, hapa tulipo kiukweli hakuna serikali ni katiba mbovu tu iliyowekwa na haohao CCM.

Dhamana iliyopo sasa ni kwa jeshi na vyombo vingine vya ulinzi kuhakikisha kipindi hiki kinapita kwa utulivu na amani bila ya kukosa haki.Hili linalofanywa na tume ya uchaguzi iliyowahusishamakada wa CCM watupu na sasa inadaiwa kuhusishwa pia vyombo vya uslama vya Taifa, hayo yanafanywa na CCM,wasimamizi wa Tume ya uchaguzi Pemba tayari wameshagundulika ni kutoka usalama wa Taifa,unategemea nini ? Maana hawa wamefanywa watumwa na CCM na sio serikali.

Kitakacho tokea Pemba kama tume ikijitia upofu sio kiachwe Pemba peke yake kiwepo Tanzania nzima kama alivyosema mgombea mmoja wa Uraisi, Wapemba au Zanzibar hawaidai haki hio kwa ajili yao bali kwa ajili ya Tanzania nzima, tusika na kuukalia uchumi kama alivyosema Mwalimu Nyerere,uchumi mnaukalia, hapa ni umoja kwa Watanzania wote wapenda amani, utulivu na haki, tuungane na Wapemba ikiwa Tume ya CCM haitasikia madai, kilichotokea Pemba kimetokea Tanzania nzima
 
Mosi: Atakaye vunja amani na usalama atachukuliwa hatua iwe Pemba, iwe wapi

Pili: Muuche kujidanganya kuwa mnaogopwa

Tatu: Muache kujifariji kuwa mtaungwa mkono
Pemba hatuna haja ya kuungwa mkono, tupo vizuri na tutapambana. Ikiwa 2001 kuna baadhi ya askari polisi walikatwa vichwa (kama ulikuw hujui hii fuatilia undani wake) usitegemee miaka hii ambapo muamko umezidi mtatazamwa tu, hawatakufa au kujeruhiwa raia peke yao na upande wa pili utaface same consequences.
 
Unafurahia kufanya vurugu!...kinukisheni lakini msije makajutia
 
Unafurahia kufanya vurugu!...kinukisheni lakini msije makajutia
Mkuu sote tunaomba mambo yaende kwa amani kubwa sana hakuna anaefurahia vurugu. Lakini kwanini wenye dola waanzishe chokochoko za makusudi, lengo ni nini hasa kana si kuvuruga amani. Ebu tuache siasa pembeni tuangalie haya mazingira yaliojitokeza, kweli kabisa inawezekana wabunge wote wa ACT wazalendo pemba yaani wao tu wawe na mapungufu na wakose sifa ya kugombea?
Vyama vingapi vipo vya siasa vipo halafu unakuja kuwaengua wabunge wote wa ACT, huo ni uchokozi wa makusudi na hautavumiliwa.
Mkuu katika historia tangia dunia iumbwe haijawahi kutokea hata siku CCM kupata mbunge hata mmoja pemba kwenye boksi la kura.
 
Mkuu kwani wewe utakuwa umehamia Serbia? Nadhani wengi huwa hatuelewi kuwa kukitokea vurugu huwa haichagui wahanga ndio maana Akwilina RIP angetosha kuwa mfano kwa wavivu wa kufikiri.
Unafurahia kufanya vurugu!...kinukisheni lakini msije makajutia
 
Kwani wapemba si walikimbia nchi.au mnauwezo wa kupigana na jeshi
 
Mosi: Atakaye vunja amani na usalama atachukuliwa hatua iwe Pemba, iwe wapi

Pili: Muuche kujidanganya kuwa mnaogopwa

Tatu: Muache kujifariji kuwa mtaungwa mkono
Kwanini tufikie huku sasa? Hatujawahi kuwa na mambo ya kuambizana kuogopwa nchini kwetu, inchi yetu imejingwa katika misingi ya haki na amani, kwanini raia wanadhurumiwa haki yao kikaktiba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…